DRC (Beni) : Shambulio jingine la waasi wa ADF limewauwa makumi ya watu eneo la Banande-Kainama

DRC (Beni) : Shambulio jingine la waasi wa ADF limewauwa makumi ya watu eneo la Banande-Kainama

Waasi wa kundi la silaha la (ADF) wamefanya shambulio jingine la mauwaji usiku wa jumanne kuamkia jumatano katika kijiji cha Vido eneo la Banande-Kainama kanda ya Beni-Mbau katika wilaya ya Beni Kivu ya kaskazini mashariki mwa DRC.Waasi hao waliwauwa kikatili raia 11 kwa kutumia silaha zisizokuwa za moto. HABARI ya SOSMedias Burundi

Mbali na kuwauwa watu, mashirika ya kiraia yanafahamisha kuwa nyumba zaidi ya 20 zilichomwa moto na wapiganaji wa ADF. Jonas Zawadi, kiongozi wa mashirika la kiraia eneo hilo anahakikisha kuwa wananchi walihama vijiji vilivyolengwa na kukimbilia sehemu ambapo wanaona usalama ni wa uhakika.

“Waasi waliingia kijijini majira ya 11 na nusu jioni siku ya jumaanne. Wananchi walikimbilia katika maeneo tofauti kwa ajili ya usalama wao. Kwa sasa matokeo ni raia 11 kuuwawa” aliwambia wenzetu wa radio Moto Oicha.

Mashirika ya kiraia yanafahamisha kuwa msako unaendelea kutafuta walionusurika au miili ya watu wengine waliouwawa wakati wa shambulio hilo. Hata hivyo eneo la Batangi-Mbau daima katika wilaya ya Beni-Mbau, madhara ya shambulio la wapiganaji wa ADF katika kijiji cha Kota Okola jumatatu iliyopita iliongezeka.

Wakati wa mwanzo, viongozi eneo hilo na waakazi walifahamisha kuwa ni watu 14 waliouwawa. Mashirika ya kiraia katika kijiji cha Mamove walifahamisha kuwa miili ya watu 6 iligunduliwa mchana wa jumanne karibu na kijiji cha Tapi-Rouge na Mambume. Wakaazi sehemu hiyo wanasikitishwa n’a visa vya usalama mdogo kurejea katika wilaya ya Beni na kulaani “Uzembe wa viongozi wa kijeshi kuhusu kutilia maanane tahadhari za wananchi”. Upande wake, Allain Siwako mbunge aliyechaguliwa katika wilaya ya Beni anafamisha kuwa katika mwezi wa septemba peke, ni watu 216 waliouwawa katika mashambulio ya waasi eneo la beni Kivu ya kaskazini, Mambasa na Irumi mkoani Ituri.

Anasikitika kwamba waasi wa ADF wanapita Kijiji hadi kingine wakifanya ukatili na vikosi vya usalama bila kushughulika .”Vijiji vingi vinaendelea kuhamwa na wakaazi wake kutoka na hali ya usalama unaozidi kuwa mbaya wakati ambapo wilaya hizo mbili ziko katika hali ya hatari tangu mei 2020 sawa na uamzi wa rais wa Kongo kwa lengo la kumaliza kabisa wakundi ya silaha ya nje na ndani ya nchi” alieleza mbunge huyo akiwa na majonzi.

Next Burundi : Chama cha CNL kimezuiliwa kuandaa siku maluum ya vijana