Makamba: Vijana Imbonerakure wahamishwa nje ya shule ya Makamba

Makamba: Vijana Imbonerakure wahamishwa nje ya shule ya Makamba

Wazazi wa wanafunzi wa shule ya kipili ya Makamba iliyo kwenye makao makuu ya mkoa huo (kusini mwa Burundi) walijiridhisha baada ya kundi la Imbonerakure (Wafuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD tawi la vijana) kuhamishiwa nje ya shule hiyo. Walikuwa kwenye shule hiyo kwa kipindi cha miezi mitano wakipewa mazoezi ya kijeshi. HABARI ya SOS Médias Burundi

Vijana Imbonerakure walipata mafunzo ya kijeshi tangu aprili.Walihamishwa katika majumba ya uwanja wa “Nkurunziza Park stadium Complex wiki iliyopita.Wazazi walilalamika juu ya malezi ya watoto wao. Wanafunzi walikuwa wamechoshwa na mazoezi ya kijeshi ya vijana Imbonerakure waliokuwa yanafanyika mchana na usiku.

” Imbonerakure hao walikuwa wakifanya mazoezi ya kijeshi, wakiwa na vifaa vinavyofanana na silaha usiku na mchana.Tulikuwa hatuwezi kusoma wala kulala kwa utulivu tukiwa shuleni.” wanafunzi walifahamisha.

Wanazidi kuwa Imbonerakure hao walikuwa wanafanya doria usiku maeneo ya pembeni ya shule. Hali hiyo iliwatia woga wanafunzi na kutothubutu kutoka nje ya mabweni nyakati za usiku kwenda kujisaidia.Baadhi ya wazazi wa wanafunzi walihakikisha kuwa “tulikuwa na wasi wasi”.

Walikuwa na hofu ya kufikisha tatizo hilo la usalama na nidhamu ya wanafunzi katika mikutano. Kiongozi wa shule hiyo André Nininahazwe alikuwa mufuasi mashuhuri wa chama tawala.wanalaani kuona mafunzo hayo yaliandaliwa na kufanyika katika eneo ambako kuna vijana wamvulana.

Wazazi walikuwa na hofu kuwa watoto wao wa kike wangebakwa. Wanaomba rais wa jamuhuri kupiga marufuku mazoezi ya kijeshi ndani ya shule na kuandika hilo katika kanuni za nidhamu.Ma mia ya Imbonerakure walikuwa wanafanya mafunzo ya kijeshi na kulala kwenye shule ya Lycée Makamba tangu aprili aliyopita.

Mbunge wa zamani na muasi Jean Baptiste Nzigamasabo marufu Gihahe, mwenye asili ya mkoa wa Kirundo (Kaskazini mwa Burundi) ndiye aliyekuwa ameteuliwa na chama cha CNDD-FDD kufuatilia shughuli hizo tangu kuanza.

Tarehe 27 agosti, katibu mkuu wa CNDD-FDD alifahamisha kuwa chama tawala kitatoa mafunzo ya kufanya gwaride ya kijeshi kwa vijana Imbonerakure elfu 25 hadi mwaka ujao. Ilikuwa katika Siku maluum ya Imbonerakure, iliyoadhimishwa mkoa ni Gitega makao makuu ya siasa.

Imbonerakure zinatajwa na UN kama kundi la waasi. Ripoti nyingi zinasema kuwa wanachukuwa nafasi za polisi, jeshi na vyombo vya sheria katika maeneo mengi ya nchi.Na tangu disemba 2021, vijana hao wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD wanajumuika na jeshi la Burundi Kivu ya kusini (Mashariki mwa DRC) ili kukabiliana na makundi ya waasi ya Warundi likiwemo kundi la Red Tabara linalichukuluwa na viongozi wa Burundi kama kundi la kigaidi kwa mjibu wa vyanzo vyetu na ripoti za mashirika yasiyoegamia upande wowote.

Tangu miezi michache iliyopita, mafunzo yao ya kijeshi hayafanyiki kwa uficho, yanaandaliwa chini ya jina la “Mafunzo ya uzalendo”

Previous Cibitoke : Zaidi ya waasi wa Rwanda 40 waliuwawa na jeshi la Burundi
Next Burundi: the dry season threatens the country, the government to implores God