Burundi: ICC yafikia hatua nyingine

Burundi: ICC yafikia hatua nyingine

Mahakama ya uhalifu wa kivita ICC inafahamisha kuwa uchunguzi nchini Burundi unaendelea vizuri na kwamba unaelekea kukamilika. Hatua inayofuata ni kutoa waranti wa kimataifa dhidi ya watuhumiwa. Mawakili watetezi wa waathiriwa wanasema kuridhika hata kama njia bado ni ndefu. HABARI SOS Médias Burundi

Miaka mitano baada ya kuanza uchunguzi kuhusu maovu yaliyotendeka nchini Burundi katika mzozo wa kisiasa wa 2015, ICC inatuliza.

” Uchunguzi unatakiwa kufanyika kwa makini ikizingatiwa kuwa watafiti hawana haki ya kukanyaga kwenye ardhi ya Burundi. Kwa hiyo kukusanya ushahidi katika mazingira hayo sio rahisi. Lakini tunahakikisha kuwa kazi ilifanyika vizuri, muda mfupi ujao tutaingia katika hatua inayofata”. Wanathibitisha hayo wajumbe wa tume ya wachunguzi ambao hawakutaka kutoa maelezo zaidi ” habari za siri” ili tusiharibu kazi ya ofisi ya mwendeshamashtaka wa ICC.

Makosa sita yaliorodheshwa na ofisi ya mwendeshamashtaka

” Ni mauwaji na jaribio la kuuwa, kufunga watu na kuwanyima uhuru, unyanyasaji, ubakaji na watu kupotea kiholela” , taarifa zinasema.

” Inakadiriwa kuwa watu 1200 angalau waliuwawa, ma mia ya wengine walipelekwa jela kinyume cha sheria na kunyanyaswa huku wasiojulikana walipo wakikadiriwa kwa mia. Vuguzu hizo zilisababisha watu 413.490 kutoroka makaazi yao kati ya aprili 2015 na mei 2017″, inafahamisha ofisi ya mwendeshamashtaka wa mahakama ya ICC yenye makao yake The Hage Uholanzi.

ICC inafahamisha hatua itakayofuata: ” Kutoa waranti wa kimataifa wa kukamatwa kwa watuhumiwa wa makosa hayo”, kulingana na kamati ya uchunguzi bila kutoa maelezo zaidi.

” Maovu hayo yalitendwa na maafisa wa serikali pamoja na makundi mengine yanayotekeleza sera ya serikali ikiwemo polisi ya taifa, idara ya ujasusi na vikosi vya jeshi vinavyofanya kazi kwa ushirikiano na vijana Imbonerakure tawi la vijana la chama tawala”, inazidi kusema ofisi ya mwendeshamashtaka.
” Mwendeshamashtaka wa ICC halazimishwi kujihusisha peke na maovu yaliyoorodheshwa ndani ya ripoti lakini ana haki ya kurefusha uchunguzi wake na kuangalia makosa mengine kama mauwaji ya kuangamiza na maovu mengine yanayoshughulikiwa na mahakama hiyo ( mauwaji ya halaiki na ya kivita) “, inahakikisha hata hivyo ICC.

Uamzi wa ngazi wa awali ulioruhusu uchunguzi huo ufanyika katika mwezi wa oktoba 2017 unafahamisha wakati na mahala ambapo uchunguzi huo utafanyika.

” Uchunguzi utahusu maovu yaliyotendeka kwenye ardhi ya Burundi na yale yaliyofanywa na watu wa nchi hiyo nje ya Burundi. Aidha kuhusu wakati, uchunguzi huo unahusu maovu yaliyofanyika kati ya tarehe 26 aprili na Oktoba 26 mwaka 2017, lakini muda unaweza kurefushwa na kuhusu maovu yaliyotendeka katika kipindi kingine au yale yaliyoendelea kutendeka” , inafahamisha ofisi ya mwendeshamashtaka wa mahakama ya ICC.

Mawakili waridhika.

Mashataka yaliyopelekwa katika mahakama hiyo kwa kiwango kikubwa yaliwasilishwa na mawakili wenye asili ya Burundi, wanaharakati wa mashirika ya kiraia wajumbe wa ” shirikisho la mawakili kwa ajili ya haki nchini Burundi ” au CAVIB, shirikisho la mawakili wa wahanga wa maovu yanayoshughulikiwa na mahakama za kimataifa ambayo yalitendeka Burundi”.

Wataalam hao wanasema kuridhishwa na hatua iliyopigwa katika uchunguzi huo kuhusu Burundi.

” Sisi pia tulikuwa hatuna mashaka. Tunafahamu kuwa ofisi ya mwendeshamashtaka inafanya kazi ngumu laki vizuri. Watafiti hawalali, wanakutana na waathiriwa, manusura, watu walioguswa na maovu yaliyotendeka nchini Burundi ambao wako katika maeneo tofauti ya hifadhi ” alieleza wakili Lambert Nigarura mjumbe wa shirikisho la mawakili.

” Wako na taarifa zote. Walifanya pia uchunguzi wa maelezo tuliyowapatia . Ofisi ya mwendeshamashtaka ina kila kitu ili kufikia hatua nyingine, ambayo ni hiyo ya kutoa waranti za kimataifa” , anatumai wakili Nigarura ambaye pia ni mratibu wa muungano wa mashirika kwa ajili ya ICC, CB-CPI

Hata hivyo, wengi wanasema kuwa muda wa uchunguzi uliochukuliwa na ICC ni mrefu, zaidi ya miaka mitano na walianza kupoteza matumaini.

” Muda wa kusubiri umekuwa mrefu na kuna uwezekano matunda yakawa si mazuri. Vidonda vyetu kufuatia ubakaji na unyanyasaji kamwe havitapona” wanahakikisha baadhi yao.

Upande wao mawakili watetezi wanawatuliza.

” Ni kweli miaka mitano inaweza kuonekana kama kipindi kirefu kwa waathiriwa wanaosuburi kutendewa haki lakini ukiangalia mkakati uliochukuliwa na ICC ikizingatiwa kuwa Burundi ilijiondoa kwenye mahakama hiyo, kipindi hicho kinaeleweka ili kukusanya taarifa zote zinazohitajika”, mawakili wanafahamisha.

Waathiriwa wengine wanahofia kuwa kuna hatari faili ya Burundi ikawa kama ile ya Ivory Cost ambapo watuhumiwa wakuu rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo na waziri wake wa zamani wa vijana Charles Blé Goudé walitakaswa na korti hiyo baada ya kukosa ushahidi wa kutosha dhidi yao.

Maoni ya mawakili ni tofauti.

” Faili ya Burundi inatofautiana sana na ile ya Cote d’Ivoire, kwanza kabisa ni kuhusu aina ya maovu yaliyotendeka na pia ni kuhusu watuhumiwa na mashtaka dhidi yao. Tuna uhakika kuwa faili ya Burundi itafikia kwa kuwapeleka mahakamani watuhumiwa maovu yaliyofanyika tangu 2015 na kuwapa fidia waathiriwa” , alimalizia wakili Lambert Nigarura.

Tangu tarehe 27 oktoba mwaka wa 2017, Burundi ilijiondoa katika mkataba wa Roma uliounda mahakama ya ICC.
Hata hivyo, korti hiyo inakuwa na mkakati wakati nchi inakuwa imejiondoa.

” kuna njia tofauti : watuhumiwa wanaweza kujipeleka wenyewe kwenye ICC au kukamatwa wakiwa safarini. Waranti zinaweza pia kutolewa na kusalia siri hadi siku ya kukamata mtuhumiwa. Watu wanaweza kulindwa za serikali lakini hali hiyo sio milele” alifafanua Fadi El Abdallah msemaji wa ICC.

Gitega upande wake inatuhumu mahakama hiyo kuegamia upande mmoja na kushirikiana na maduwi wa Burundi na waliofanya mapinduzi ili kuharibu sura ya Burundi.

Akiulizwa juu ya habari hizo, waziri wa sheria alijizuia kutoa maelezo yoyote.

” Natumai ambaye anaweza kuwapa maelezo zaidi ni msemaji wa serikali ambaye pia ni katibu wake” , alijibu msemaji wa wizara ya sheria, Donavine Niyongere

Previous Muyinga: residents give their contributions in the week of the war veterans, the collections end up in the individuals' pocket
Next Meheba (Zambia): soaring market prices