Tanzania : viongozi tawala wawahamasisha wakimbizi kuhusu kuheshimu sheria ambazo wao wanazikiuka kila mara

Tanzania : viongozi tawala wawahamasisha wakimbizi kuhusu kuheshimu sheria ambazo wao wanazikiuka kila mara

Wiki mbili zilitumiwa kuwahamasisha kuhusu sheria za nchi na zile zinazowahusu wakimbizi ndani ya kambi za Nduta na Nyarugusu. Wakimbizi waligundua kuwa wanalindwa na sheria nzuri lakini nchi iliyowapa hifadhi ikisumbuka kuzitekeleza. HABARI SOS Médias Burundi

Kampeni ya kuwahamasisha iliandaliwa na mahakama kuu ya kanda ya kigoma (kaskazini magharibi mwa Tanzania), uongozi wa kambi, polisi pamoja pia na idara ya uhamiaji.

Lengo ni kwa ajili ya kupunguza idadi ya wakimbizi wanaopokekwa jela.

” Tulipita katika magereza ya kanda ya Kibondo na Kisulu na tuligundua kuwa kuna wakimbizi miongoni mwa wafungwa hususan warundi. Baadhi yao wanajitetea kuwa hawajuwi sheria. Kupitia haya, tunataka mufahamu kuhusu makosa ya jinai na adhabu yake”, maafisa wa Tanzania walifafanua.

Wakimbizi wanadai kuwa sheria ni nzuri kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi wao.

” Hakika, sheria zilitungwa vizuri. Tulisikia kuwa tuko na haki ya kutembea hadi kilometa sita nje ya kambi katika vijiji vya karibu na kambi, na ni jambo nzuri kwa ajili ya kupunga upepo na hata kufanya biashara ndogo ndogo na kuimarisha uhusiano na jamii iliyotupa hifadhi”, walibaini wakimbizi wa kambi ya Nduta.

Tatizo kulingana mkimbizi huyo ni utekelezwaji wa sheria.

” Fikiria kuwa hata mtu aliyekamatwa akiwa ndani ya kijiji kinachogusa kwenye kambi zetu aliadhibiwa kwa tuhma za kutoka nje ya kambi bila idhini. Harafu biashara zilipigwa marufuku hapa wakati ambapo makao makuu ya mji yanatambuliwa na sheria ambazo tulifundishwa” wakimbizi walalamika.

Visa viwili vilichukuliwa kwa umakini katika kambi ya Nduta.

Msichana mkaazi wa zone 15 village 6 nambari 70, alinyanganywa maharagwe yake yenye uzito kilogramu 82 kwa tuhuma kwamba anamiliki shamba nje ya kambi pasina kutoa ushahidi. Harafu mwanaume mkaazi wa zone 13, village 12 na mambari 30 aliona kitunga chake cha vitumbua kikichukuliwa na polisi ambayo pia ilimusimamisha kwa tuhuma za kwenda kunuwa unga nje ya kambi kwa lengo la kufanya biashara haramu. Kwa hiyo wanatufundisha sheria ambazo na wenyewe hawaheshimishi”. wakimbizi wenye hasira walilaani.

Wakaazi hao wa kambi za Nduta na Nyarugusu wanakosoa vikali hatua ya kitu na kinyume chake.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliyoambatana na viongozi tawala katika kampeni hiyo ya kuwahamasisha wananchi, yalitoa wito kwa wakimbizi kupeleka mashtaka kwenye mashirika hayo kila mara wanaopohisi kuwa wamenyanyaswa au wakati wakiwa kwenye mgogoro na sheria.

Ma kundi ya mawakili kwa ajili ya kutetea haki za wakimbizi yataundwa kwa ushirikiano na mashirika ya kiutu likiwemo la DRC (Danish Refuheey Council), jambo ambalo linawapa moyo wakimbizi licha ya kupoteza matumaini na kufahamisha kuwa hawajataraji ni kitu kikubwa kutokana kwa juhudi hizo.

Tanzania inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi laki mbili wakiwemo laki moja na elfu 45 kutoka Burundi.

Previous Burundi: Mashirika yasiyokuwa ya hisani yalazimishwa kutoa nauli viongozi tawala ili kuwasili uwanjani
Next Uvira : zaidi ya watu wengine 300 kutoka Burundi wakimbilia nchini DRC