Uvira : zaidi ya watu wengine 300 kutoka Burundi wakimbilia nchini DRC

Wanapewa hifadhi katika kambi ya muda ya Sange ndani ya wilaya ya Uvira mkoa wa kivu-kusini (mashariki mwa DRC) tangu siku chache zilizopita. Wahusika ni kutoka hususan katika mikoa ya Cibitoke na Bubanza (kaskazini magharibi mwa Burundi). HABARI SOS Médias Burundi

Warundi hao wanadai kuwa walifukuzwa ndani ya ardhi zao na serikali.

” Serikali yetu ilitunyanganya ardhi zetu. Hakuna haki ya kwenda katika mashamba yetu. Kilichosalia kwetu ni kukimbia” walilaani wajumbe wa kundi kundi hilo waliozungumza na SOS Médias Burundi.

Ardhi hizo zinazozungumziwa zinapatikana eneo la Mabayi, Nyarure, Rugombo, Mbazamiduha katika mkoa wa Cibitoke pamoja na Kibira-Rukoko mkoani Bubanza.

Mmoja kati ya viongozi wa kambi hiyo ya muda ya Sange anafahamisha kuwa takriban waomba hifadhi hao wote, wanakutania katika hoja moja : Kunyanganywa ardhi zao”.

Kuhusu swala hilo, gavana wa mkoa wa Cibitoke anapinga madai hayo. Carême Bizoza anafahamisha kuwa serikali ilirejesha ardhi ambazo zilikuwa miliki yake. Anatoa mifano ya ardhi za Nyarure na Mbazamiguha.

Mkoani Bubanza, gavana anasema ni eneo ambako kunafanyika mazoezi ya kijeshi.

Lakini waomba hifadhi hao kutoka Burundi ” wanadai ni ukiukwaji wa haki zao”.

Katika miaka ya hivi karibuni, walishuhudiwa warundi wanaokimbilia nchini RDC kutokana na njaa mbali na wale waliokimbia kutokana na unyanyasaji dhidi ya wapinzani lakini hii imekuwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati kuwapokea watu wenye asili ya Burundi kwa idadi kubwa wanaotoroka kwa sababu ya Kunyanganywa ardhi za kilimo.

Previous Nduta (Tanzania) : kijana mkimbizi kutoka Burundi alipatikana akiwa maiti baada ya kukosekana
Next Uvira: another more than 300 Burundians find refuge in DRC