Uvira (DRC): Wakongo wanalalamika kuwa soko la ajira limevamiwa na Warundi

Uvira (DRC): Wakongo wanalalamika kuwa soko la ajira limevamiwa na Warundi

Wakongo wanaofanya kazi katika ujenzi, biashara, madereva wa pikipiki, teksi za baiskeli, wasusi wa nywele, wahudumu wa mikahawa, wafanyikazi wa nyumbani, au hata mawakala wa kuhamisha pesa, wanasema kwamba Warundi wengi huenda Uvira kuchukua sekta hizi. Iko katika jimbo la Kivu Kusini mashariki mwa DRC.

HABARI SOS Media Burundi

Shoshi ni Mkongo, yuko kwenye ujenzi. Kulingana naye, karibu nyumba zote za Uvira kwa sasa zimejengwa na Warundi “kwa sababu wanaomba pesa kidogo kuliko sisi”.

Paul ni mwendesha pikipiki. Anakadiria kuwa huko Uvira, kuna zaidi ya waendesha baiskeli elfu moja wa Burundi.

Wakikabiliwa na mmiminiko wa idadi kubwa ya Warundi wanaokuja kutafuta kazi nchini Kongo, mashirika ya kiraia yana wasiwasi. Kwake, wanachukua kazi ya Wakongo na hii inaweza kusababisha ukosefu wa usalama. Hivi karibuni, wawakilishi wake katika kanda waliandaa maandamano dhidi ya Burundi.

Mratibu wa Jumuiya ya Kiraia Mpya ya Kongo, Mafikiri Mashimango akizungumza na wafanyabiashara na Meya wa mji wa Uvira, alisema sababu iliyowafanya kuandamana ni idadi kubwa ya raia wa Burundi wanaoendelea kuingia Kongo na kufanya biashara nchini kwa njia zisizo halali.

“Wafanyabiashaŕa wadogo wana matatizo ya kuuza, na hali hii ina madhaŕa hasi kwa usalama wa mji wa Uvira. Ndio maana tuliandamana hadi kwa meya wa jiji kwa sababu hakuna sheria inayomruhusu mgeni kuwa mchuuzi mitaani. Waweke wafanyabiashara hawa wa Burundi kwenye soko la Kilomoni (Kavimvira-mpakani).”

Kulingana na baadhi ya wafanyabiashara wa Kongo, wimbi kubwa la wafanyabiashara wa Burundi katika Uvira limesababisha mauzo yao kushuka. Hivyo, kulipa kodi pamoja na kodi ya stendi na nyumba za biashara kumekuwa tatizo.

Wafanyabiashara wa Burundi huenda katika mji wa Uvira kila siku kuuza maji, maziwa, mboga, viatu, nguo, nyama, vinywaji na bidhaa nyinginezo.

Muuzaji wa Burundi wa mishikaki iliyochomwa huko Uvira

Kulingana na warundi hawa wanaokuja kwa wingi kufanya biashara nchini Kongo, ni soko zuri kwa sababu bidhaa zao zinauzwa kirahisi hapa nchini.

Uwimana, mwanamke mwenye umri wa miaka 40 tuliyekutana naye katika kituo cha biashara cha Mulongwe, anauza maji. Anasema kwamba Wakongo pia wanauza bidhaa zao nchini Burundi bila tatizo.

“Pia tuna haki ya kuuza bidhaa zetu nchini Kongo kwa sababu tuko katika jumuiya moja ya C.E.P.G.L*,” anajitetea.

Ijapokuwa Warundi wanakuja kwa wingi kutafuta kazi nchini Kongo, wanasema wanateswa na polisi wanaowachukulia kama wezi, waasi na wahamiaji wasio na vibali.

Meya wa Uvira, Kiza Muhato alitangaza kuwa anakusudia kuunda kamati ya wafanyabiashara kuchunguza taratibu za kufungua tena soko la Kilomoni ambapo wafanyabiashara wa mitaani wa Burundi wangeweza kuuza bidhaa zao, karibu na mpaka na Burundi.

—————-

Mfanyabiashara wa mtaani wa Burundi huko Uvira

Previous Tanzania: UNHCR inajaribu kuwatuliza wakimbizi wa Burundi
Next Kirundo: Mchungaji wa kanisa anayeshukiwa kwa ujasusi kizuizini

You might also like

Criminalité

Ituri: Raia 25 wauawa katika shambulizi la ADF huko irumu

SOS Médias Burundi Irumu, Januari 26, 2026 – Wanamgambo kutoka Allied Democratic Forces (ADF) walishambulia tena kijiji cha Apakolu, katika eneo la chifu la Walese Vonkutu eneo la Irumu katika

DRC Sw

Goma: Maaskofu wa Kikatoliki na wawakilishi wa kanisa la Kiprotestanti waliwatembelea mabwana wapya na kuwasihi kuwe na mazungumzo jumuishi.

Baraza la Maaskofu wa Kongo (Cenco) na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC) Jumatano lilitoa wito kwa pande zinazohusika katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC,

DRC Sw

DRC – Rwanda: Wanafunzi wa Kongo na Rwanda waonyesha usawa katika elimu kati ya nchi hizo mbili licha ya kutofautiana kwao

Mvutano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda uliibuka mwaka wa 2022 wakati mgawanyiko mkubwa ulipozuka kati ya mataifa haya mawili katika eneo la Maziwa Makuu barani Afrika.