Kabarore: walimu walazimishwa kutoa michango
Walimu katika tarafa ya Kabarore mkoa wa Kayanza (Kaskazini mwa Burundi) walilazimishwa kutoa michango ya pesa ili kufadhili miradi ya chama tawala cha CNDD-FDD. Wahusika wanatupilia mbali kile wanachoita “ukiukwaji wa haki za binadamu”. HABARI ya SOS Medias Burundi
Tangu mwaka wa 2015, walimu katika baadhi ya tarafa za Kayanza wanalazimishwa kutoa michango kwa nguvu ili kufadhili miradi ya chama tawala nchini Burundi. Tarafani Kabarore, walezi hawachangii tena.
Vyanzo vyetu katika walimu wanatuarifu kuwa michango hiyo ni ya kila mwezi.
Walimu wakuu wa shule za msingi wanatoa kati ya 5000 na 10000 sarafu ya Burundi kutokana na idadi ya wanafunzi kwenye shule hiyo.
“Sisi walimu tunatoa elfu moja au elfu mbili. Kwa kipindi fulani walitulazimisha kutoa elfu 3 sarafu za Burundi, alieleza mwalimu.
Jambo la kusikitisha kwa mjibu wa walimu, hakuna anayeepukika.
“Hata wafuasi wa vyama vingine wanahusishwa”, anahakikisha mwalimu mwengine.
Wanaopinga kuchukuliwa kama wasiokuwa na utu.
“Mara tunaitwa mbwa , mara tunapewa jina la mbwa mwitu”, alithibitisha mwalimu mufuasi wa chama cha upinzani.
Walimu wanasema kuchoshwa na michango hiyo hasa ikizingatiwa kuwa hawajuwi inapoelekea pesa hiyo.
“Hakuna matokeo kutoka kwenye michango yetu”, analaani mwalimu mkuu wa shule, mufuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD.
Walimu waliojieleza kwenye SOS Medias Burundi wanataja kuwa kuchangisha kwa nguvu ni “ukiukwaji wa haki za binadamu”. Wanaomba serikali na viongozi wa chama cha CNDD-FDD kwa ngazi ya taifa kuingilia kati na kusimamisha mwenendo huo.
Viongozi wa elimu katika mkoa wa Kayanza, hawakupatikana ili kujieleza juu ya madai hayo.
You might also like
Chama Florina chahitimisha Kampeni Yake Rugombo Ikilenga Kilimo na Uvuvi
SOS Médias Burundi Rugombo, Juni 2, 2025 — Akifunga kampeni zake za uchaguzi katika tarafa ya Rugombo, katika Mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi) Jumapili hii, Rais wa Chama cha
Geneva: ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye mstari unaopanda nchini Burundi
Tangu Juni 18, Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa limefanya kikao chake cha 56. Itakamilika Julai 12. Wiki iliyopita, Burundi ilikuwa kwenye ajenda na ripota wa Umoja
Burundi: Mashirika yasiyokuwa ya hisani yalazimishwa kutoa nauli viongozi tawala ili kuwasili uwanjani
Washirika wanaohudumu katika maeneo yoyote ya nchi sasa wataanza kuandaa bajeti kwa ajili ya kugharamia ziara za viongozi tawala. Hayo ni kwa ajili ya kuwawezesha kufika uwanjani kukagua hatua iliyopigwa
