Burundi: Mashirika yasiyokuwa ya hisani yalazimishwa kutoa nauli viongozi tawala ili kuwasili uwanjani
Washirika wanaohudumu katika maeneo yoyote ya nchi sasa wataanza kuandaa bajeti kwa ajili ya kugharamia ziara za viongozi tawala. Hayo ni kwa ajili ya kuwawezesha kufika uwanjani kukagua hatua iliyopigwa katika kutekeleza wa miradi. Uamzi huo ulichukuliwa jumatatu hii katika mkutano kati ya waziri mkuu Gervais Ndirakobuca na magavana wa mikoa.
Wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya serikali wanasema ni aina ya rushwa inayohalalishwa. HABARI SOS Medias Burundi
Katika baadhi ya mikoa, magavana tayari wameanza kuwapa taarifa wahusika. Mfano ni katika tarafa ya Rumonge kusini magharibi mwa nchi.
Gavana wa mkoa huo aliitisha mkutano na washirika hao wa kiufundi na kiuchumi wanaohudumu katika mkoa huo baada ya kikao na waziri mkuu mjini Gitega ( jiji kuu la siasa)
Consolateur Nitunga aliwambia kuwa sasa wataanza kufadhiri ziara zao wakiwasili uwanjani lakini pia na zile za wakuu wa tarafa.
Lengo la ziara hizo za viongozi ni kushuhudia miradi na hatua za utekelezwaji wa miradi ya mashirika hayo yasiyokuwa ya kihisani.
Washirika hao wa kiufundi na kiuchumi wanalazimika kutangaza rasmi kiwango cha pesa iliyotengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi katika eneo fulani. Hayo ni kwa ajili ya kupata urahisi katika kupanga bajeti inayotakiwa ili kuwawezesha viongozi tawala kuwasili uwanjani.
Mashirika hayo yanatakiwa kuonyesha wazi miradi inayotekelezwa ndani ya kila tarafa ou mkoa.
Hatua hiyo imekosolewa na wawakilishi wa mashirika hayo yasioyokuwa ya kiserikali mkoani Rumonge. Baadhi walitangaza kuwa ni aina ya rushwa iliyohararishwa. Wanazidi kuwa baadhi ya magavana wa mikoa huwalazimisha wasimamizi wa miradi kuwapa kiwango fulani cha pesa pasina sababu yoyote. Wengine huomba kiwango kikubwa cha mafuta ya gari huku mafuta hayo mara baada ya kutolewa yanaishia kwenye soko la kienyeji la bidhaa hiyo.
Washirika hao wanahakikisha kuwa hali hiyo itasababisha madhara makubwa katika utekelezwaji wa miradi ya maendeleo hasa kwamba hakuna mfadhiri hata mmoja anayeweza kupanga bajeti kwa ajili ya kuwapa nauli viongozi wanaowasili uwanjani.
Wanadai kuwa ni jambo lisiloeleweka kufadhi mradi pamoja anayenufaika na mradi wenyewe.
Ifahamike kuwa katika mkutano huo wa waziri mkuu na wakuu wa mikoa wa tarehe 17 oktoba, sekta nne zilipewa kipau mbele.
Sekta hizo ni afya, maji safi na usanifishaji, kilimo, ufugaji na mazingira pamoja pia na elimu na utamaduni, utawala bora na haki za binadamu.
You might also like
Burundi: Upinzani wasusia na mivutano inayozunguka mchakato wa uchaguzi kabla ya 2027
SOS Médias Burundi Bujumbura, Mei 9, 2026 — Huko Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi na nyumbani kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali kuu, mchakato wa uchaguzi
Usambazaji wa kadi za uchaguzi: wakazi walio katika matatizo kaskazini-magharibi, kuongezwa kwa tarehe ya mwisho iliyoombwa
SOS Media Burundi Cibitoke, Mei 14, 2025 – Mwishoni mwa usambazaji wa kadi za uchaguzi, wananchi wa mikoa ya Cibitoke, Bubanza na Bujumbura, kaskazini-magharibi mwa Burundi, wanakashifu utendakazi katika mchakato
Cibitoke: Ndirakobuca Ahakikisha — “Burundi haitarudi kwenye mfumo wa chama kimoja”
SOS Médias Burundi Cibitoke, Juni 14, 2025 – Wakati CNDD-FDD ilishinda viti vyote katika uchaguzi wa wabunge na manispaa wa Juni 5, Waziri Mkuu wa Burundi Gervais Ndirakobuca mnamo Ijumaa
