Bubanza: Mbunge Fabien Banciryanino aibua mjadala

Bubanza: Mbunge Fabien Banciryanino aibua mjadala

Katika sherehe za kuomboleza mauwaji ya rais Melchior Ndadaye, mbunge wa zamani Fabien Banciryanino aliweka shaada za mauwa ambako ameandika kuwa demokrasia ilidaiwa na Ndadaye haijaonekana. Jambo hilo limeibua mjadala. HABARI SOS Medias Burundi

Vyama vingi vya kisiasa, viongozi tawala mkoani Bubanza (magharibi mwa Burundi) pamoja na mbunge wa zamani wa kujitegemea Fabien Banciryanino waliweka shaada za mauwa kukumbuka shujaa wa demokrasia miaka 29 baada ya kufariki kwake.

Banciryanino amekuwa wa mwisho kuweka mauwa ambako imeandikwa na herufi kubwa ” Demokrasia ulioacha hatujaanza kunufaika na matunda yake”)

Mandishi hayo yamesababisha mjadala kwa wanasiasa, polisi na viongozi waliohudhuria sherehe hizo.

Mkuu wa kijiji cha Bubanza Jean Marie Nyabenda, imborakure ( mjumbe wa tawi la vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD) mwenye ushawishi mkubwa ambaye alikuwa akisimamia sherehe hizo, ametoa maneno dhidi ya mbunge huyo anayejulikana kama mtu asiye jikawusha kusema.
Alisema kuwa Fabien Banciryanino hakuelewa maana ya demokrasia. ” ataelewa badaye tathmini ya neno demokrasia” amesisitiza mkuu huyo wa kijiji.

Mkuu wa polisi ngazi ya mkoa naye amejiingiza ndani. Amechukuwa hata picha ya mandishi hayo. Jambo hilo halikumusikitisha bwana Banciryanino.

” Hata kama wangejaribu kunikataza kuweka mauwa hayo, hilo halingeniumiza”, amesema mbunge huyo aliyefungwa jela kati ya oktoba 2020 na oktoba 2021 akituhumiwa kufanya uasi na kuvuruga usalama wa ndani ya nchi” kutokana na kauli yake wakati alipokuwa muwakilishi wa wananchi katika jumba la mikutano ya bunge la Kigobe ( kaskazini mwa jiji kuu la kibiashara la Bujumbura) ambako vinafanyika vikao vya wabunge.

Wakaazi wa mkoa wa Bubanza wanalalamika kuwa Imbonerakure wajiingiza katika mfuno wa sheria.

” Kila siku wako tayari kukamata watu dhaifu na wapinzani” wamebaini.

” Hawakuelewa alichomanisha Ndadaye alipotaka ” demokrasia ” amesema raia mmoja.

Previous Muyinga: Zaidi ya wapinzani 50 wanazuiliwa jela
Next Burundi: Mashirika yasiyokuwa ya hisani yalazimishwa kutoa nauli viongozi tawala ili kuwasili uwanjani