DRC-Goma : serikali ya Kongo haijakuwa tayari kuzungumza na kundi la M23

DRC-Goma : serikali ya Kongo haijakuwa tayari kuzungumza na kundi la M23

Akiwa ziarani mjini Goma, waziri wa mawasiliano Patrick Muyaya aliongoza mkutano na wandishi wa habari jumatatu hii. Mahojiano na wandishi wa habari yaliangazia hali ya usalama katika eneo hilo la mashariki linalokabiliwa na ” vita vya uvamizi”. Waziri huyo alikumbusha uamzi usiobadilika wa serikali ya Kongo kuwa haiko tayari kuandika kwenye agenda yake ya shughuli za siku mazungumzo na kundi la M23. HABARI SOS Médias Burundi

Katika mkutano huo na wandishi wa habari, waziri huyo wa Kongo alisema kuwa ni magaidi.

” Hatutazungumza kamwe na magaidi sababu hatuwezi kukubali vurugu. Tayari tulikuwa katika mchakato wa mazungumzo wa Nairobi ” , alihakikisha waziri huyo wa mawasiliano na vyombo vya habari.

Akijieleza kuhusu matamshi ya rais wa Rwanda Paul Kagame kuhusu hali inayojiri mashariki, waziri wa mawasiliano katika tamko hilo anaona ndani yake kuwa utawala Kigali unaelekea kuanguka.

” Mwenendo wanaoonyesha ni mwenendo unaoashiria kuanguka. Kuna utashi mkubwa hususan kwa ngazi ya mpatanishi mkubwa ambaye ni rais wa Angola pamoja na rais wa Burundi, tuna matumaini kuwa kupitia njia hiyo, suluhu litapatikana”, alithibitisha Patrick Muyaya. Hata hivyo alizidi kusema kuwa serikali ya Kongo inatakiwa kukaa na nchi zinazounga mkono makundi ya silaha yanayosambaratisha nchi hiyo.

” Tunatakiwa kuangalia swala hilo mtambuka, tuko na ADF , tuko na M23. Kwa kipindi fulani tutalazimika kuzungumza na nchi za makundi hayo ili kuangalia namna ya kuyashughulikia hata kama rais wa Rwanda hataki kukubali. Anatakiwa kujihusisha na FDLR ni wananchi wake. Sisi hapa hatuwataki kwa sababu wamekuwa chanzo cha vurugu na tunataka wananchi wetu waweze kuishi katika amani. Hatutaki wawe wakimbizi ” alieleza Patrick Muyaya.

Kwa kukumbushia, waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari aliwasili mjini Goma akiambatana na ujumbe wa rais wa Uswizi uliokuja mjini Goma kwa ajili ya kazi za kibinadamu.

Kundi la M23 ni kundi la zamani la waasi wa kabila la watutsi. Lilichukuwa silaha mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kuacha kutekeleza ahadi zake kuhusu kuwarejesha katika maisha ya kiraia wapiganaji wake. Tangu kundi hilo kuibuka, viongozi wa Kongo wanakubaliana kuwa linapata msaada kutoka Rwanda, madai ambayo serikali ya Rwanda inazidi kutupilia mbali .

Upande wake, Rwanda inatuhumu viongozi wa Kongo kushirikiana na kundi la waliotekeleza mauwaji ya halaiki nchini Rwanda la FDLR kwa kuwapa sare , silaha na risasi kwa lengo la ” kuvuruga ardhi ya Rwanda”.

Previous Burundi : waziri mkuu wa zamani Alain Guillaume Bunyoni huenda alitoroka nchi, maafisa wawili wa polisi wakamatwa
Next Rutana-Giharo : viongozi wa chama tawala walazimisha wapinzani kutoa michango kwa ajili ya siku kuu yao