Burundi : waziri mkuu wa zamani Alain Guillaume Bunyoni huenda alitoroka nchi, maafisa wawili wa polisi wakamatwa

Burundi : waziri mkuu wa zamani Alain Guillaume Bunyoni huenda alitoroka nchi, maafisa wawili wa polisi wakamatwa

Tangu jumatatu hii, vyanzo mbali mbali mjini Bujumbura (mji mkuu wa kiuchumi) vinaeleza kuwa huenda aliyekuwa waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni alitoroka nchi. Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, huenda alielekea katika nchi jirani ya Tanzania. Maafisa wawili wa polisi wenye cheo cha kanali wasimamishwa na idara ya ujasusi. HABARI SOS Médias Burundi

Vyanzo vingi vya karibu na waziri mkuu wa zamani vinasema kuwa huenda alitoroka nchi. Hii ni baada ya kupata taarifa za uwepo wa mpango wa kukamatwa kwake, kulingana na vyanzo vyetu.

” Mkutano ukifanyika mkoani Cibitoke ( Kaskazini magharibi) . Washiriki walipanga kumkamatwa Bunyoni lakini habari zilivuja. Baada ya hayo, alichukuwa hatua ya kukimbia nchi” chanzo cha karibu na ofisi ya rais kiliambia SOS Médias Burundi.

” Hatuna uhakika wa njia aliyokamata, lakini mara ya mwisho alikuwa mkoani Rutana ” vyanzo vya polisi vilieleza kwa kujificha.

Walinzi wake wa zamani wanathibitisha habari hizo. Wanazidi kuwa tajiri wao wa zamani alielekea nchini Tanzania.

” Hadi sasa ni siku nyingi pasina kuwaona ma dereva wetu wa zamani waliovuka mpaka pamoja na Bunyoni” walihakikisha.

Kukamatwa kwa maafisa wawili wa polisi

Ma kanali wawili wa polisi ikiwa ni pamoja na Désiré Uwamahoro kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia (BAE) na Alfred Innocent Museremu kiongozi wa upelelezi wa nje katika idara ya ujasusi hadi jumatatu iliyopita, walikamatwa na kuhojiwa na idara ya upelelezi. Wa pili aliachiwa huru. Alirejelewa na kanali Pierre Claver Nzisabira ambaye hadi wakati huo alikuwa katibu wa kudumu wa baraza la usalama. Maafisa hao wawili walitajwa kuhusika na visa ukiukwaji wa haki za binadamu wakati na baada ya mandamano ya 2015 dhidi ya muhula wa kutatanisha wa hayati rais Pierre Nkurunziza.

Gatoni Rosine Guilene msemaji wa raia Ndayishimiye ambaye ofisi yake inahusika kuwateuwa viongozi wa idara ya ijasusi hakupatikana ili ajibu maswali yetu. Désiré Nduwimana msemaji wa polisi amesema kuwa alikuwa katika mapumziko kutokana na ugonjwa.

Jumatatu hii, makaazi mawili ya aliyekuwa waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni yamelengwa na msako wa polisi na idara ya ujasusi katika mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura na mkoani Rutana kusini mashariki mwa Burundi eneo la asili la wazazi wake na ambalo linapakana na Tanzania.

” Kama inavyokuwa ada, ninadai kuwa faili kuhusu Bunyoni, imefufuliwa na Neva, ili kuelekeza macho ya warundi kwenye faili hiyo wakati huu ambapo kipau mbele ni majanga ya kiuchumi ambapo rais Ndayishimiye anatajwa pamoja na mke wake na watoto wake. Ndayishimiye hawezi kutoa amri ya kutafuta vitita vikubwa vya pesa kwake Bunyoni. Kwa mtazamo wangu, sio kwa njia hiyo ambapo wanafuatilia watuhumiwa wizi wa mali ya umma. Kuna ujanja katika mwenendo huo. Aidha kuhusu uwezekano wa Bunyoni kutoroka nchi, siwezi kushangaa nikisikia kuwa amesalia Bujumbura kwa sababu, Bunyoni bado ana ushawishi mkubwa katika kwa wafuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD” ni tathmini yake Bob Rugurika kiongozi wa Radio Publique Africaine ambaye wakati huu anaishi uhamishoni.

Previous Masisi: mapigano makali kati ya kikosi cha Burundi na kundi la M23
Next DRC-Goma : serikali ya Kongo haijakuwa tayari kuzungumza na kundi la M23