Masisi: mapigano makali kati ya kikosi cha Burundi na kundi la M23

Masisi: mapigano makali kati ya kikosi cha Burundi na kundi la M23

Mapigano makali ya kundi la M23 dhidi ya wanajeshi wa Burundi wa kikosi cha jumuiya ya Afrika mashariki yalifanyika siku ya ijumaa. Jeshi la Kongo linahakikisha kuwa zaidi ya wapiganaji 10 wa kundi la M23 waliuwawa na wengine kukamatwa. HABARI SOS Médias Burundi

Ni mchana wa ijumaa ambapo mapigano hayo yaliibuka. Yalifanyika eneo la Jérusalem katika kitongoji cha Malehe katika wilaya ya Masisi. Msemaji wa kikosi cha kikanda cha EAC alifahamisha katika tangazo siku ya ijumamosi kuwa mapigano yaliendelea hadi usiku na jumamosi asubuhi.

” Mapigano yaliibuka wakati wapiganaji wa M23 walitaka kudhibiti tena baadhi ya ngome walizoacha wiki kadhaa zilizopita. Wanajeshi wa Burundi wajumbe wa kikosi cha kikanda wanaohudumu eneo hilo, walipinga hilo”, yanaeleza mashirika ya kiraia eneo hilo.

Habari hizo zimethibitishwa na jeshi la Kongo katika mkoa wa Kivu kaskazini. Jeshi hilo linahakikisha kuwa angalau wapiganaji 10 waliuwawa, wengine walikamatwa pamoja na zana za kijeshi.

” Tunapongeza ushujaa wa wanajeshi wa Burundi walifungua moto kwa ajili ya kuwalinda wananchi dhidi ya uvamizi wa M23. Wananchi wanahitaji amani” , alibaini luteni kanali Guillaume Ndjike Kaiko msemaji wa gavana mwanajeshi wa mkoa wa Kivu kaskazini.

Mashirika ya kiraia ya ndani yanaripoti kuwa yaliona gari za kubeba wagonjwa sikifanya nenda rudi kwa ajili ya kuchukuwa maiti na majeruhi waliokuwa wamevalia sare za kijeshi , wengine nguo za kawaida ambao idadi yao na uraia bado kujulikana.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa kikosi cha EAC kilichotumwa nchini DRC kupigana dhidi ya M23.

Upande wake, kundi la M23 halijasema chochote kuhusu mapigano hayo ya waasi wake dhidi ya wanajeshi wa Burundi.

Kulingana na makubaliano ya Luanda ( Angola) na Nairobi (Kenya) , kundi la M23 liliahidi kuacha ngome zake za zamani na kuzikabidhi kikosi cha EAC tangu disemba 2022.

Lakini katika baadhi ya maeneo, vyanzo vyetu vinasema kuwa kuna uvunjaji wa amri hiyo ya kusitisha vita inayoendelea. Burundi ina kikosi vitatu vilivyotumwa kwenye ardhi ya nchi hiyo kubwa jirani wa magharibi. Walitumwa katika mkoa wa Kivu ya kusini na Kivu kaskazini katika jukwa la ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili na chini ya mwamvuli wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Previous RDC (Ituri) : angalau wananchi 40 waliuwawa na waasi wa CODECO
Next Burundi : waziri mkuu wa zamani Alain Guillaume Bunyoni huenda alitoroka nchi, maafisa wawili wa polisi wakamatwa

About author

You might also like

DRC Sw

Burundi: kuelekea uandikishaji wa usawa wa diploma kwa wakimbizi wa Kongo

Burundi inajiandaa kuanzisha hatua kubwa ya kupendelea ushirikiano wa kijamii na kiuchumi wa wakimbizi wa Kongo katika ardhi yake: utoaji wa usawa wa diploma zao. Mpango huu unaibua matarajio makubwa

DRC Sw

Kivu Kaskazini: waandishi wa habari hatarini katika mji wa Goma

Watuhumiwa wawili wa mauaji ya Edmond Bahati, mratibu wa radio Maria-Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, waliwasilishwa kwa vyombo vya habari na idara ya upelelezi ya kijeshi siku

Usalama

Burundi: utawala wa rais Ndayishimiye unafanya mauwaji kama ule wa mtangulizi wake Nkurunziza

Shirika la kutetea haki za binadamu la Iteka linatoa tahadhari . Katika ripoti yake ya mwisho, shirika hilo la zamani kabisa la kutetea haki za binadamu nchini Burundi limetoa orodha