Rutana-Giharo : viongozi wa chama tawala walazimisha wapinzani kutoa michango kwa ajili ya siku kuu yao
Kulingana na mkuu wa chama cha CNL tarafani Giharo mkoa wa Rutana (kusini mashariki mwa Burundi), viongozi wa eneo hilo wa chama tawala walitoa mamlaka kwa Imbonerakure ( wajumbe wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD) ya kukusanya kwa nguvu vyakula na pesa kwa lengo ya kuandaa sherehe iliyopangwa kufanyika tarehe 22 aprili 2023. Viongozi wa chama cha upinzani cha CNL wanaomba viongozi tawala kuwalinda dhidi ya vitisho na kuwanyamanzisha. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mjibu wa viongozi wa chama cha upinzani cha CNL, Imbonerakure hao wanafanya mikutano kwa ajili ya kupanga zoezi la kukusanya vyakula hususan katika kijiji cha Giharo.
” Kwa zaidi ya wiki moja Ernest Niyonizeye kiongozi wa Imbonerakure katika kijiji cha Giharo hutembea maeneo yote ya kijiji hicho kutoa vitisho kwa wananchi na kutahadharisha yoyote ambaye atapinga zoezi hilo la ukusanyaji muhimu kwa ajili ya siku kuu yao” alifahamisha kiongozi wa chama cha CNL.
Vitu vinavyokusanywa ni vyakula ambavyo kwa sehemu kubwa ni mbegu za mahindi, na franka 4000 kwa kila mtu, wakisema ni kwa ajili ya kununua nguo za vijana wafuasi wa chama tawala kwa ajili ya siku kuu hiyo.
” Mazoezi ya kijeshi kwa ajili ya kuwatishia wale waliopinga nia yao yalianza tangu tarehe 7 aprili kuanzia saa kumi na mbili jioni” wanasikitika wafuasi wa chama cha upinzani.
Mbali ya zoezi hilo la ukusanyaji, Imbonerakure hao kwa ushirikiano na ma katibu wa vijiji wa chama tawala, husambaza vitisho kwa lengo la kuwalazimisha wafuasi wa chama cha CNL kujiunga na chama cha CNDD-FDD kwa ajili ya kuepuka na matatizo, viongozi wa chama cha CNL wanalalamika.
Viongozi hao wa chama kikuu cha upinzani tarafani Giharo wanamutuhumu Alexis Baraguma katibu wa chama cha CNDD-FDD katika kijiji cha Giharo, Ernest Niyonizeye mkuu wa Imbonerakure pamoja na katibu wa chama hicho katika maeneo ya mlima wa Bayaga Frédéric Nyamweru kuwa chanzo cha kufanya michango hiyo kwa nguvu.
Wanaomba viongozi tawala kuwalinda wafuasi wa vyama vya upinzani wanaotishiwa kifo na Imbonerakure hao ambao wanazidi kutoa ujumbe kuwa ” ambao watapinga mpango wao, watauwawa”.
Jumapili hii, kiongozi mkuu wa chama cha CNL alikosoa ” ujumbe wa chuki unaotolewa na katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD na hali ya kutovumiliana kisiasa inayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi”. Ilikuwa katika kongamano la wafuasi wa chama chake katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega.
Miaka iliyopita, viongozi kimkoa wa chama tawala walijulikana sana kwa kukusanya michango kwa nguvu au kujipa kwa nguvu kwa ajili ya mandalizi ya matukio ya chama chao yanayojilikana au la kwa ngazi ya kitaifa.
About author
You might also like
RDC (Ituri) : angalau wananchi 40 waliuwawa na waasi wa CODECO
Vijiji vitatu vya eneo la Banyali Kilo, wilayani Djugu katika mkoa wa Ituri mashariki mwa DRC vililengwa na mashambulizi ya wakati mmoja ya waasi wa CODECO (shirikisho kwa ajili ya
Goma: zaidi ya wakazi 17,000 wapya waliohama makazi yao kutokana na vita kati ya jeshi la kawaida na waasi wa M23
Zaidi ya watu 17,000 waliokimbia makazi yao wamesajiliwa katika kambi mpya iliyoundwa katika mji wa Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini (mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo). Kulingana na
Kesi-Bunyoni : sheria nchini Burundi yafunga akaunti za waziri mkuu wa zamani
Benki kuu ya Burundi BRB ( benki ya jamuhuri ya Burundi) ilitoa amri kwa mashirika ya fedha yote ili yasiruhusu kuondoa au kuweka pesa kwenye akaunti za waziri mkuu wa