Kakuma (Kenya) : maradhi ya usafi mdogo yatishia waomba hifadhi

Kakuma (Kenya) : maradhi ya usafi mdogo yatishia waomba hifadhi

Maradhi ya usanifishaji mdogo yanashuhudiwa kwenye kituo cha mapokezi ya waomba hifadhi ndani ya kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya . Kituo kicho kimeathirika zaidi kutokana na msongamano wa watu na udogo wa eneo hilo. Msimu wa mvua ulikuja kuhatarisha mazingira. HABARI SOS Médias Burundi

Kituo cha mapokezi katika kambi ya Kakuma kaskazini magharibi mwa Kenya kimezidiwa na idadi kubwa ya waomba hifadhi. Maradhi yanayotokana na usafi mdogo yanaanza kushuhudiwa.

” Kituo kicho kinachopatikana katika maeneo ya viillage ya Kakuma III kimeathiriwa pakubwa sababu kinahifadhi zaidi ya watu elfu tatu katika maeneo madogo yaliyoandaliwa ili kupokea watu. Kufuatia mvua nyingi inayonyesha katika kanda ya Turkana mnamo siku hizi, vyoo viliharibika”, alisikitika mfanyakazi wa kujitolea wa HCR.

Katika eneo la Kalobeyei ambako kuna kituo cha kupanua kambi ya Turkana, vituo vitatu vipya vilifunguliwa.

” Eneo hilo pia ni hali kadhalika na mazingira ya maisha yanafanana. Kadiri watu wanakuwa wengi, ndivyo wanavyokosa maji safi, na hivyo maradhi ya usanifishaji mdogo huingia na kushambulia hasa watoto “, walisisitiza wadau eneo hilo.

Waomba hifadhi wapya katika kambi ya Kakuma kwa sehemu kubwa ni wenye asili ya nchi ya DRC, Somalia na Sudan kusini. Kwa hao, wanajumulika pia wale kutoka Burundi walitoroka kambi za wakimbizi nchini Tanzania na Uganda wakitafuta mazingira mazuri ya maisha kwa mjibu wao.

Wanaomba HCR kuharakisha mchakato wa kuwapa hadhi ya ukimbizi ili waweze kuingia katika village na Blocs za kambi.

Wakimbizi wengine upande wao waliomba HCR kuweka pembeni wagonjwa ambao tayari walipatikana na ugonjwa wa kuharisha ili kuthibiti mambukizi ndani ya kambi hiyo inayowapa hifadhi watu zaidi ya laki mbili wakiwemo warundi elfu 25.

Previous Rutana-Giharo : viongozi wa chama tawala walazimisha wapinzani kutoa michango kwa ajili ya siku kuu yao
Next Burundi : tume ya haki za binadamu imethibitisha kukamatwa kwa Bunyoni