Bujumbura: watendaji watatu wa rais wahamishiwa katika gereza la Mpimba
Jean Baptiste Baribonekeza, mkuu wa zamani wa Tume Huru ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu, CNIDH, Cyrille Sibomana na Arcade Harerimana, waliwasili katika gereza la Bujumbura linalojulikana kwa jina la Mpimba mwendo wa saa 8:40 mchana.
HABARI SOS Médias Burundi
Wanaume hao watatu walikuwa wamezuiliwa katika seli za Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (SNR) tangu siku ya kukamatwa kwao, Alhamisi iliyopita. Mashahidi waliiambia SOS Médias Burundi kwamba watendaji watatu wa ofisi ya rais wa Burundi waliwasili Mpimba mwendo wa saa 8:40 mchana.
https://www.sosmediasburundi.org/2025/01/09/bujumbura-trois-cadres-de-la-presidence-burundaise-detenus-par-les-renseignements/
“Wote watatu walifika hapa, wakiandamana na maafisa wa hati hawakuwa wamevaa mikanda,” shahidi aliyewaona wakiingia gerezani.
Shirika la Kupambana na Ukosefu wa Ajira na Mateso, ALUCHOTO, kilifuatilia kwa karibu oparesheni ya kuondoa msongamano wa magereza. Anaendelea kukashifu shughuli iliyojaa dosari nyingi.
“Tunadai kwamba wale wote waliohusika katika shambulizi lililozingira oparesheni ya kufungua magereza waadhibiwe vikali,” alitangaza Ijumaa iliyopita, Vianney Ndayisaba, mwakilishi wa shirika hili ya ndani, katika mkutano na waandishi wa habari ambao alisimamia katika mji mkuu wa kiuchumi, Bujumbura .
———
Sehemu ya gereza kuu la Bujumbura lijulikanalo kwa jina la Mpimba ambapo watendaji watatu wa ofisi ya rais wa Burundi wamekaa tangu jioni ya Januari 12, 2025, DR.
About author
You might also like
Nyanza-Lac: wanaume watatu walikamatwa na kupelekwa kusikojulikana
Wanaume watatu walikamatwa Jumamosi hii, Mei 18, na mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (SNR) ya Nyanza-Lac na kamishna wa polisi wa mkoa, baada ya upekuzi nyumbani kwao. Sababu
DRC (Beni) : watu zaidi ya kumi wauwaw a katika shambulio jingine la kundi la ADF eneo la Rwenzori
Watu 13 waliuwawa katika shambulio jingine ya waasi wa AFD (nguvu zilizoungana kwa ajili ya demokrasia) katika usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa . Shambulio hilo lilifanyika katika kitongoji cha Bukokoma
Makamba: mahabusu alifia kwenye selo ya ofisi ya mwendesha mashtaka wa mkoa
Jérôme Ndikuriyo alifariki mapema asubuhi ya Jumanne hii katika seli ya mwendesha mashtaka wa Makamba (kusini mwa Burundi). Alikuwa mgonjwa kwa muda lakini hakupewa ruhusa ya kutafuta matibabu. HABARI SOS