Kivu-kaskazini : watetezi wa haki za binadamu wako hatarini katika maeneo ya migogoro ya silaha
Watetezi wa haki za binadamu katika wilaya ya Rutshuru wanatahadharisha kuhusu vitisho dhidi yao kutoka kwa viongozi wa makundi ya waasi. Wanatoa takwimu za wanaharakati 18 waliouwawa na makundi ya silaha katika kipindi cha miezi mitatu. HABARI SOS Médias Burundi
Katika tamko la jumanne hii eneo la kiwanja wilayani Rutshuru ndani ya mkoa wa Kivu-kaskazini ( mashariki mwa DRC), watetezi wa haki za binadamu wanadai kuwa wanalengwa na makundi ya silaha yanayoendesha operesheni zake katika eneo hilo la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Hayo ni tangu kuanza kwa mapigano kati ya jeshi la RDC na waasi wa M23 ndani ya wilaya za Rutshuru na Masisi , katika mkoa wa kivu kaskazini.
Kwa mujibu wa Patrick Ricky Paluku kiongozi wa shirika la haki za binadamu katika wilaya ya Rutshuru, angalau wanaharakati 18 waliuwawa katika kipindi cha miezi mitatu peke.
” Ni hali isiotoa utulivu kwetu, sisi watetezi wa haki za binadamu katika wilaya ya Rutshuru. Makundi ya silaha yanatushambulia na tunajiuliza lini hali hiyo itamalizika. Katika kipindi cha miezi mitatu peke, wenzetu 18 waliuwawa na makundi ya silaha katika vitongoji viwili vya wilaya ya Rutshuru baada ya kulaani maovu yanayotekelezwa na makundi ya waasi”, alibaini.
Uongozi wa mashirika ya kiraia, Forces vive de Rutshuru, unahakikisha kuwa waasi wa M23, pamoja na wajumbe wa CMC Nyatura, Mai Mai na waasi wengine eneo hilo, wote yamekuwa chanzo cha mauwaji ya wanaharakati.
Viongozi wa makundi ya silaha yaliyotajwa hapo awali, yanatuhumiana kuhusu madai hayo ya mashirika ya kiraia.
” Ni wajumbe wa muungano wa serikali ya Kinshasa, CMC Nyatura, Mai-Mai na FDLR. Wanatekeleza mauwaji ya wananchi na watetezi wa haki za binadamu kwa lengo la kuharibu sura yetu. Wanaficha ishara za ushirikiano wao na hivyo kushambulia ngome zetu lakini pia raia wanaozungumza Kinyarwanda” alituhumu meja Willy Ngoma msemaji wa kundi la M23.
” Hatuwezi kuwauwa wananchi waliotupa uaminifu wao na ambao tunalazimika kuhakikishia usalama asubuhi, mchana na usiku na tunawalinda kama inavyotakiwa” alizidi kusema msemaji wa kundi la M23.
Akijieleza, Jules Muomba mmoja kati ya wasemaji wa makundi ya ndani, anawahusisha waasi wa kundi la M23.
” Tulijiunga katika kundi mmoja ili kutetea wananchi wetu ambao wanaathiriwa na uvamizi dhidi ya mkoa wetu. Hakika ni waasi wa M23 wanaowauwa wananchi” alibaini Jules Mulumba.
Tangu mapigano kuanza katika eneo la mashariki mwa nchi, wilaya ya Rutshuru imekuwa eneo la mauwaji ya wananchi wa kawaida.
Wiki iliyopita, zaidi ya wakaazi kumi waliuwawa katika eneo la Bungushu katika kijiji cha Bwito ndani ya wilaya ya Rutshuru kwa mujibu wa mbunge aliyechaguliwa katika jimbo hilo. Eneo la janga hilo liko chini ya udhibiti wa kikosi cha kanda cha EAC.
Mteule huyo anatuhumu wanajeshi wa EAC kikosi cha Kenya, Uganda na Sudani kusini kushirikiana karibu na waasi wa M23.
” ni jambo lisiloeleweka kuona watu wakiuwawa katika eneo chini ya udhibiti wa kikosi cha kikanda. Tunaomba hatua kali zichukuliwe ili kumaliza kabisa hali ya usalama mdogo “, alisisitiza.
Zaidi ya watu 100.000 walitoroka makaazi yao na ma kumi ya wengine kuuwawa katika mashambulizi ya makundi ya silaha ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini, mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (RDC) lilieleza mwezi machi shirika la umoja wa mataifa.