Cibitoke : watu watano wenye asili ya Rwanda wanaobebelea silaha waliuwawa katika mapigano na jeshi la Burundi ndani ya msitu wa Kibira

Cibitoke : watu watano wenye asili ya Rwanda wanaobebelea silaha waliuwawa katika mapigano na jeshi la Burundi ndani ya msitu wa Kibira

Milio ya silaha nzito ilisikika tangu ijumaa iliyopita ndani ya msitu wa hifadhi wa Kibira kwenye milima ya Gasenyi na Gafumbegeti tarafani Mabayi mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi). Kwa mujibu wa wanajeshi wanaofanyia kazi katika msitu huo, waasi watano wa Rwanda waliuwawa. Wakaazi wa maeneo ya karibu wanasema kuwa wamejawa na hofu. Wanaomba usalama uweze kuimarishwa. Mwanajeshi wa cheo, anayehusika na operesheni za jeshi katika tarafa za Mabayi na Bukinanyana anawatuliza wananchi hao. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na vyanzo katika taasisi za usalama, wakati wa doria ndani ya msitu wa Kibira, wanajeshi walifungua moto na kuwapiga risasi kundi la watu wenye silaha wanaochimba madini kinyume cha sheria ndani ya msitu huo. Watano kati yao waliuwawa na wanne walijeruhiwa vikali.

Miili ya waliofariki ilitambuliwa. Ni wajumbe wa kundi la silaha wanaozungumza Kinyarwanda ambao wamepiga kambi eneo hilo kwa kipindi cha makumi ya miaka.

Walizikwa ndani ya msitu huo siku ya jumatatu. Majeruhi wanapata matibabu ndani ya hospitali moja ya mjini Bujumbura, mji mkuu wa kibiashara.

Kati kati ya mchana, siku hiyo ya jumatatu, muili wa mwanajeshi mmoja wa Burundi uligunduliwa eneo hilo pamoja na wanajeshi wengine wawili waliojeruhiwa vikali. Walipelekwa mjini Bujumbura.

Taarifa kutoka maeneo hayo zinasema kuwa kuna kundi la watu wenye silaha lililojipa kazi ya uchimbaji madini na biashara ya mbao kutoka miti ya msitu huo.

Milio hiyo ya risasi ilisababisha hofu kubwa kati ya wananchi wakaazi wa maeneo ya karibu na msitu huo.

Hii ni baada ya kundi la silaha kutoka Rwanda la FLN kuripotiwa ndani ya msitu huo baada ya zaidi ya miezi miwili ya utulivu. Vyanzo eneo hilo vinaarifu kuwa kundi hilo linajiandaa kutekeleza shambulio dhidi ya Rwanda.

Afisa wa jeshi wa cheo anayehusika na operesheni za jeshi anawatuliza wananchi. Anawahakikishia usalama wananchi wakaazi wa tarafa za Mabayi na Bukinanyana.

Hata hivyo, anatahadharisha kuwa hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia ndani ya msitu kwa ajili ya kufanya shughuli yoyote. Kuna hatari ya kumufananisha na watu wanaobebelea silaha.

Previous Uvira : watu wawili wauwawa
Next DRC - Rutshuru : usalama wazidi kuwa mbaya katika kitongoji cha Busanza