Uvira : watu wawili wauwawa
Watu hao ni wanaume wawili wa jamii ya Banyamulenge. Waliuwawa na watu wanaobebelea silaha ambao wanadaiwa kuwa ni waasi wa kundi la Mai Mai jumapili hii alasiri. Kisa kilitokea katika eneo la Kirungu, wilayani Uvira mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC. HABARI SOS Médias Burundi
Wahanga hao walikuwa wakitoka katika mji wa Uvira wakielekea eneo la Minembwe huku wakitumia barabara ya Uvira-Kirungu-Bijombo.
Ruyenzi Kavuganyi alikuwa mkaazi wa kitongoji cha Bizimana wakati ambapo Rigean Rumaraninda akiishi katika kitongoji cha Nyabigugu.
Waliuwawa na watu wenye silaha ambao walidaiwa kuwa waasi wa kundi la Mai Mai-Makanaki.
” Watu hao wawili waliuwawa wakati wakitembea na miguu. Waasi waliowamalizia maisha, walikuwa wakivalia sare za jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo)”, mashahidi wamesema.
Kwenye barabara hiyo, angalau watu 5 wajumbe wa jamii ya Banyamulenge waliuwawa na watu wa makundi ya silaha ya ndani kwa mjibu wa mwakilishi wa shirika moja la eneo hilo.
” Ni jambo la kusikitisha na mauwaji hayo ninayachukuwa kama mauwaji ya kuvizia sababu ni watu wa jamii ya Banyamulenge wanaolengwa wakati ambapo Bafulero, Bashi, Bavira wanaosafiri pamoja nao, wakiwa hawaguswi “, analaani Musore, msafiri anayetumia barabara ya Uvira-Kirungo-Bijombo.
” Pamoja na hayo, watu hao wameuwawa wakiwa karibu na kizuwizi cha wanajeshi. Mara nyingi, wanauwawa baada ya kuwalipa wanajeshi lakini wanajeshi hao hawawashindikizi kwa ajili ya kuwalinda”, vyanzo vyetu viliendea kwa sharti ya kuhifadhi majina yao. Wahanga hao wa siku ya jumapili waliuwawa karibu ya kizuwizi cha jeshi.
Watu wengine wawili walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo la jumapili dhidi ya wasafiri hao wawili. Majeruhiwa ni askali polisi wawili wajumbe wa jamii ya Banyamulenge pia.
Rutabara Sengambi na Rugazura walikuwa hawana silaha wakati walipovamiwa”, vyanzo vyetu vinasema.
Msemaji wa jeshi la FARDC katika jimbo la Kivu kusini hakupatikana ili kujibu maswali yetu kadhalika yule wa kundi la Mai Mai-Makanaki.
Kati ya 2017 na 2022, angalau wajumbe wa jamii ya Banyamulenge 1500 waliuwawa nchini Kongo kwa mujibu wa wanaharakati wanaotetea haki za watu wa jamii hiyo ambao kwa sehemu kubwa inaundwa na wafugaji.
Wanaharakati hao wanasema kuwa ” Mauwaji hayo yanachukuwa mueleko wa mauwaji ya kikabila kuelekea mauwaji ya kuangamiza ama jenoside”.