DRC – Rutshuru : usalama wazidi kuwa mbaya katika kitongoji cha Busanza

DRC – Rutshuru : usalama wazidi kuwa mbaya katika kitongoji cha Busanza

Wakaazi wa kitongoji cha Busanza ndani ya kijiji cha Bwisha wilayani Rutshuru mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo walaani kuona visa vya usalama mdogo vikiendelea kushuhudiwa mnamo siku hizi katika baadhi ya maeneo ambako kunaripotiwa waasi wa M23 na makundi ya silaha ya ndani. Vyanzo mbali mbali vinasema kuwa uwepo wa makundi hayo mawili yanayozozana, huchangia katika kuleta hali ya usalama mdogo ndani ya maeneo hayo. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mujibu wa vyanzo eneo hilo, mapigano kati ya kundi la M23 na makundi ya silaha na waasi eneo hilo yanafanyika takriban kila siku. Baadhi ya wananchi hukimbia na kwenda nchini Uganda wakati wengine wakielekea kwenye makao makuu ya wilaya ya Rutshuru.

” Kutokana na hali hiyo, shughuli za kijamii na kiuchumi zilisimama tangu miezi kadhaa. Mbali na hayo, maeneo hasa ya : Ruharashi, Kaitorea, Changwi, Kitagoma na Kavugizo yanaathiriwa zaidi na visa vya ubakaji, wizi wa mali, utekaji nyara dhidi ya wananchi. Wakimbizi wa ndani ” wanadai kuwa serikali ya Kongo iliwasahau “.

Wakimbizi hao wanaoishi kwenye mpaka baina ya Kongo na Uganda wanaomba viongozi wenye nguvu kuhusishwa ili amani iweze kurudi katika maeneo hayo ya mkoa wa Kivu kaskazini.

Previous Cibitoke : watu watano wenye asili ya Rwanda wanaobebelea silaha waliuwawa katika mapigano na jeshi la Burundi ndani ya msitu wa Kibira
Next Burundi : nchi imeorodheshwa katika nchi za kwanza ambako rushwa imekithiri