Burundi : nchi imeorodheshwa katika nchi za kwanza ambako rushwa imekithiri

Burundi : nchi imeorodheshwa katika nchi za kwanza ambako rushwa imekithiri

Maadhimisho ya siku ya Afrika dhidi ya rushwa tarehe 11 julai 2023 : hakuna maendeleo makubwa kwa mujibu wa OLUCOME (shirika la kupambana na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya uchumi nchini Burundi). Taasisi za utawala zinatakiwa kuzingatia hatari iliyopo kutokana na vitendo vya rushwa na kuchukuwa hatua zinazostahili ili kukabiliana na hali hiyo, amefahamisha kiongozi wa shirika hilo la zamani ya kupiga vita vitendo vya rushwa katika nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki. HABARI SOS Médias Burundi

Katika mkutano na wandishi wa habari jumanne hii mjini Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi, kiongozi wa shirika la kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya uchumi nchini Burundi amefahamisha kuwa Burundi inaendelea kuanguka tangu mwaka wa 2005 licha ya kuidhinisha mkataba wa Afrika kuhusu kupiga vita rushwa. Mkataba huo uliidhinishwa na serikali miaka 20 iliyopita .

Nchi 48 za Afrika ziliidhinisha mkataba huo kuhusu kuimarisha vita dhidi ya rushwa mjini Maputo( Musumbiji). Gabriel Rufyiri anasema kuwa matokeo ya vita hivyo si ya kuridhisha hususan nchini Burundi.

” Tangu mwaka wa 2005 ( mwaka ambapo chama cha CNDD-FDD kiliingia madarakani) hadi sasa Burundi inaendelea kurudi nyuma kwa mujibu wa vigezo vya shirika la transparency International. Mwaka wa 2005, Burundi ilikuwa kwenye nafasi ya 130 kwa jumla ya karibu nchi 167 na alama ya asilimia 23. Mwaka wa 2022, nchi iko kwenye nafasi ya 171 kwa jumla ya nchi 180 na alama ya asilimia 17″ amefahamisha.

Kulingana na kiongozi huyo wa OLUCOME, maovu yanayosisitizwa ndani ya mkataba wa bara la Afrika kuhusu visa dhidi ya Rushwa yamekithiri ndani ya nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki.

” Ninazungumzia makosa kama kutajurika bila sababu, kuhalalisha bidhaa zilizotokana na rushawa[…] . Tunaomba wafanyakazi wa ummaa kuheshimisha utaratibu unaowazuia kuchanganya majukumu yao na shughuli zingine”, alisisitiza.

Madhara ya rushwa kulingana na Rufyiri ni makubwa : Nchi inaingia katika vurugu kirahisi, watumishi wa umma wanakuwa wabinafsi, hali inayokuwa kikwazo kwa maendeleo ya kiuchumi. Kwa mjibu wa mwanaharakati huyo, iwapo hali haitabadilika, itasababisha matumaini kupotea kwa rika zijazo “.

” Katika mazingira ambapo vyombo vya habari na mashirika ya kiraia hawana ruhsa ya kupata taarifa zote zinazoficha rushwa, kama unavyozungumzia mkataba, shirika la OLUCOME linaomba uwazi zaidi katika kuratiba shughuli za umma”, anadai kiongozi wa shirika hilo . Rufyikiri aligundua kwa rushwa imekithiri ndani ya jamii ya Afrika kwa jumla na hususan nchini Burundi ambako kuna haja ya kufanya mageuzi haraka ya taasisi za nchi. Kwa mujibu wake , ni budi kuajiri viongozi wakuu, kutathmini upya utaratibu wa kutoa masoko ya uzabuni, kutofautisha mihimili,….).

Burundi, DRC na Sudan ndio nchi za jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) zinazoorodheshwa katika nchi 10 za kwanza duniani ambako vitendo vya rushwa vimekithiri. Rwanda imewekwa kwenye orodha ya nchi wanafunzi wazuri kulingana na shirika la transparency International.

Kulingana na kamati ya uchumi ya umoja wa mataifa kwa ajili ya Afrika, visa vya rushwa vinasababisha hasara ya bilioni 148 dola kwa mwaka katika bara la Afrika.

Nchi ya kwanza kwa rushwa inapatikana barani Afrika kwa mujibu wa Transparency International . Nayo ni Somalia.

Previous DRC - Rutshuru : usalama wazidi kuwa mbaya katika kitongoji cha Busanza
Next Nduta (Tanzania) : mazingira magumu ya wakimbizi wa Burundi waliorudi ukimbizini