Nduta (Tanzania) : mazingira magumu ya wakimbizi wa Burundi waliorudi ukimbizini
Viongozi katika kambi ya Nduta Kaskazini magharibi mwa Tanzania wako katika sensa na kuorodhesha watoto wadogo wasiokuwa pamoja na wazazi wao. Hayo ni wakati maisha yao ni mabaya sababu hawatambuliki ili waweze kupewa misaada. Ni wajumbe wa familia za watu waliorejea ukimbizini. HABARI SOS Médias Burundi
Idadi kubwa ya watoto hao wasiokuwa pamoja na wazazi katika kambi ya Nduta ni watoto ambao walirejea ukimbizini baada ya kurudi nchini.
Hakika, watoto hao wanaishi katika majumba ya watu wa familia zao za mbali. Wazazi wao wanahofia kuwa watoto watarejeshwa nchini, wanawaacha ndani ya kambi na kwenda kukaa katika vijiji vya karibu na kambi “, wanaeleza wakimbizi.
Watoto hao wanaishi katika mazingira magumu. Mfano ni mtu mama mwenye umri zaidi ya miaka 50 aliyewapokea wajukuu wake.
” Mimi ninaishi na wajukuu wangu wenye umri kati ya 8 na 14. Waliacha mtoto wangu wa kike na mumeo ambao walirejea ukimbizini na kwa vile hawawezi kupokelewa hapa ndani ya kambi, walikwenda kupanga nyumba nje ya kambi “, alieleza . Alipendeleza jina lake lihifadhiwe kwa sababu za usalama wake.
” Kwa hiyo, kuwapa chakula ni jambo gumu bila kusema huduma zao za afya au masomo kwa sababu hawana hadhi ya ukimbizi. Tunalazimika kuchangia kidogo ninachopewa na HCR. Majirani pia baada ya kujuwa kuwa wako hapa watoto hao, wananisaidia ili kupata chakula. Nilitoa taarifa kwa HCR na kwa mashirika mengine na hakuna matokeo “, analaani huyo ambaye anasema hana chaguo jingine.
Watoto hao wanne wasiokuwa na wazazi, wameorodheshwa kupitia sensa hiyo lakini bibi yao bado amesalia bila matumaini.
” Sijuwi kitakachotokea, lakini ninatumai kuwa hawatarudisha kwa nguvu kama inavyokuwa kwa watu wazima na iwapo itakuwa hivyo, basi sheria zitakuwa zimekiukwa. Badala yake, ninaomba watoto hao wapewe hadhi ya wakimbizi ili waweze kupewa misaada “, alisema mama huyo mzee.
Idadi kamili ya watoto walioachwa na wazazi wao ndani ya kambi hadi sasa bado haijulikani lakini wanakadiriwa kuwa na ma mia mengi.
Tangu 2020, Tanzania inawapokea zaidi warundi wanaorejea ukimbizi baada ya kirundi nyumbani. Mara baada ya kuwasili kambini, wanapelekwa moja kwa moja kwenye mpaka.
” Hapa, waomba hifadhi wengi wanaishi bila kutambulika kwa hofu ya kujulikana na hivyo kurudishwa nyuma kwa mara nyingine. Wanalala katika nyumba za marafiki zao. Kwa hiyo chakula na huduma za afya ni changamoto kubwa kwao”, wanaeleza wakimbizi hao.
Wanaona kuwa ni ukiukwaji wa makubaliano kuhusu wakimbizi na waomba hifadhi.
” Tuchukuwe mfano wa familia hii ambao waliorejea mkoani Ruyigi ( mashariki mwa Burundi). Mara baada ya kuwasili, walinyanyaswa. Walimaliza usiku wakilala musituni kabla ya kuwasili katika kambi ya Nduta , kambi wanayofahamu baada ya kukaa ndani ya kambi hiyo kwa miaka 5. ” Kuwarejesha nyuma, ni aina nyingine ya kuwanyanyasa na pia ukiukwaji mkubwa wa makubaliano ya 1951 ya mjini jiniva kuhusu kulinda haki za waomba hifadhi ‘ alitoa tathmini hiyo kiongozi mmoja wa kijamii katika Kambi ya Nduta anayelaani kuwa ” HCR imeshindwa au imekuwa mshirika wa Tanzania kuhusu ukatili huo dhidi ya wakimbizi wa Burundi “.
Kambi ya Nduta inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi 76 elfu kutoka Burundi ambao wanatambuliwa na HCR.