Kayogoro : hali ya wasi wasi yawakabili wananchi kutokana na mazoezi ya kijeshi ya Imbonerakure

Kayogoro : hali ya wasi wasi yawakabili wananchi kutokana na mazoezi ya kijeshi ya Imbonerakure

Imbonerakure, wajumbe wa tawi la vijana wafuasi wa chama tawala, wanafanya mazoezi ya kijeshi hususan usiku. Mazoezi hayo yanafanyika katika vijijini vyote vya tarafa ya Kayogoro katika mkoa wa Makamba kusini mwa Burundi. Kwa mjibu wa wakaazi, katibu tarafa wa chama cha CNDD-FDD ndie anayehusika na kuandaa mafunzo, ambayo kwa mujibu wake, ni maandalizi ya maadhimisho ya siku maluum ya Imbonerakure. Na kulingana na wafuasi wa vyama vya upinzani, ni njama za kuwatishia kabla ya sensa kubaini misimamo ya kisiasa ya watu kufanyika. HABARI SOS Médias Burundi

Vijiji ambavyo hamasa kwa ajili ya kuitikia mafunzo hayo ni kubwa ni kijiji cha Bigina. Ni eneo la kuzaliwa la katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD Révérien Ndikuriyo.

Jumatatu hii, mafunzo hayo yameanza kati ya saa tisa na saa kumi za asubuhi kwenye vijiji vya 12 vya kitongoji hicho.

” Imbonerakure hao wanafanya mazoezi wakibebelea fimbo na marungu. Waandaji wa mafunzo hayo ni katibu wa chama cha CNDD-FDD ngazi ya tarafa Aloys Kadoyi na Bernard Ciza, mkuu wa Imbonerakure tarafani Kayogoro”, wanahakikisha wananchi ambao wanaonyesha pia wasi wasi wao kuhusu hali hiyo ikingatiwa kuwa hali hiyo inajiri kabla ya sensa ya wafuasi wa vyama vya upinzani kufanyika katika tarafa zote.

Wanaeleza kuwa kutokana na mafunzo hayo, baadhi ya wananchi wanaoamka mapema kwenda shambani, wanalazimika kuchelewa kwa kuhofia kuvurugwa na Imbonerakure hao”.

Kwa mujibu wa chanzo eneo la Kayogoro, baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzani walijiunga na chama cha CNDD-FDD mara baada ya sensa hiyo kutangazwa kwa kuhofia ” kupata matatizo “.

Viongozi wa chama tawala wanatupilia mbali madai hayo. Wanaeleza kuwa mafunzo hayo ni kwa lengo la kuandaa sherehe za siku maluum ya Imbonerakure ambayo itaadhimishwa hivi karibuni bila hata hivyo kueleza kwa nini mafunzo hayo yanafanyika nyakati za usiku na kila siku za kazi.

Previous Nduta (Tanzania) : mazingira magumu ya wakimbizi wa Burundi waliorudi ukimbizini
Next Burundi : ni mapema kubainika wazi madhambi ya Bunyoni