Burundi : ni mapema kubainika wazi madhambi ya Bunyoni

Burundi : ni mapema kubainika wazi madhambi ya Bunyoni

Mahakama kuu ya Burundi alhamisi hii ilifahamisha kuwa mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri anaendelea kutafuta mashtaka mapya dhidi ya Bunyoni. Msemaji wa mahakama kuu na ofisi ya mwendeshamashtaka mkuu aliyefahamisha hayo, alizidi kusema kuwa mwendeshamashtaka yuko na taarifa mpya zinazoweza kumuelekeza kwenye njia ya maovu mengine katika faili dhidi ya waziri mkuu wa zamani Allain Guillaume Bunyoni. HABARI SOS Médias Burundi

Ni katika kipindi cha wasemaji wa taasisi za umma ambapo msemaji wa mwendeshamashtaka mkuu alifahamisha hayo. Alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari wa ndani ya nchi.

“Katika awamu wa mwanzo, Bunyoni alifuatiliwa kwa kuvuruga usalama wa ndani ya nchi, kuhujumu uchumi na kutumia cheo chake kutafuta maslahi yake binafsi na kumiliki silaha kinyume cha sheria pamoja na kumutukana rais wa nchi”, alifahamisha Agnès Bangiricenge.

Alisema kuwa “mwendeshamashtaka alikataa rufaa baada ya wakili wake kupinga hatua ya kumushikilia jela kwa muda. Mwendeshamashtaka alipata habari mpya zinazoweza kumufungulia mashtaka mapya”, alisisitiza.

Mmoja kati ya waendeshaji wa kipindi alitaka kujuwa maelezo zaidi kuhusu madai ya kumiliki silaha kinyume cha sheria wakati Bunyoni akiwa askali polisi wa cheo cha jemedali.

“Ni wewe unaoona hivyo na kusema hivyo hivyo. Iwapo wamesema anamiliki silaha kinyume cha sheria, inamaanisha kuwa waligundua nyumbani kwake silaha zingine mbali na zile anazoruhusiwa kumiliki”, alijibu hivyo kwa hasira.

Mwanzoni mwa mwezi mei mwaka huu, Alain Guillaume Bunyoni alipelekwa katika gereza kuu ya Ngozi (Kaskazini mwa Burundi) baada ya kumaliza siku nyingi katika gereza la SNR (idara ya kitaifa ya ujasusi) ndani ya mji wa kibiashara wa Bujumbura.

Shirika la Human Right Watch linaomba viongozi wa Burundi kuhakikisha kesi dhidi yake inaendeshwa kwa haki na uwepo wa waangalizi wa kimataifa ili haki ya Bunyoni iweze kuheshimiwa”.

Muasi huyo wa zamani wa kihutu chini ya vikwazo vya serikali ya marekani, alifutwa kwenye wadhifa wake na rais wa jamuhuri Evariste Ndayishimiye mwanzoni mwa mwezi septemba 2022 katika mazingira ya giza.

Previous Kayogoro : hali ya wasi wasi yawakabili wananchi kutokana na mazoezi ya kijeshi ya Imbonerakure
Next Burundi : tatizo la uhaba wa mafuta, majibu yake bado kupatikana