Burundi : tatizo la uhaba wa mafuta, majibu yake bado kupatikana

Burundi : tatizo la uhaba wa mafuta, majibu yake bado kupatikana

Baada ya miezi 18 ya uhaba wa mafuta ya gari, viongozi wa Burundi hawawapi moyo wananchi. Wanachukuwa hatua zisizodumu. Wanaharakati upande wao, wanaomba mkutano mkuu ufanyike kuhusiana na tatizo hilo. HABARI SOS Médias Burundi

Nchini Burundi, linapokuja swala la uhaba wa mafuta ya gari, watu wamekata tamaa wengine wamezoea . Wananchi wanatakiwa kuzowea uhaba wa mafuta ya gari na hasa uongo na majibu ya kukwepa yanayotolewa na viongozi ambao wanazidi kuhakikisha kuwa ” ghala za Burundi zimejaa ” mjini Dar Es Salam ( Tanzania).

Ukweli huo ulikaririwa alhamisi hii na msemaji wa rais Ndayishimiye.

” Kuna waagizaji wa mafuta wasiopenda nchi ambao wanaegesha lori zao nyumbani na kukataa kwenda kuleta mafuta nchini Tanzania. Hawako juu ya sheria na sio watu wasioweza kuguswa. Idara zinazohusika zinawajibika na watu hao watapelekwa mbele ya sheria wakati wowote”, alifahamisha msemaji wa rais Evariste Ndayishimiye, Rosine Guilene Gatoni katika kipindi cha wasemaji wa taasisi za umma kilichofanyika mkoani Muramvya kati kati mwa Burundi.

Kwa mujibu wake, serikali itaangalia uwezekano wa kununua lori zake na kujiandaa kujenga ghala katika ardhi ya Burundi . Na hapa hakuna maelezo yaliyotolewa.

Kwa mujibu wa watalaamu, swala la uhaba wa mafuta ya gari ni ngumu na linaomba kujadiliwa katika mkutano mkuu.

” Ni tatizo linalodumu. Limekuwa na kawaida. Warundi wanatakiwa kuona mafuta hapa, na sio katika ghala mjini Dar Es Salam. Hata Kongo ambayo inakabiliwa na mzozo na ambayo tunasaidia katika maswala ya usalama, haina matatizo ya kuagiza mafuta ya gari”, anasema Faustin Ndikumana, kiongozi wa Parcem , shirika linalopambana kwa ajili ya utawala bora.

Wadadisi wengi wanadai kuwa tatizo la uhaba wa mafuta ya gari husababishwa na uhaba wa pesa ya kigeni, na urasibu mbaya.

Previous Burundi : ni mapema kubainika wazi madhambi ya Bunyoni
Next Nyarugusu (Tanzania) : mauwaji ya mkimbizi kutoka Kongo anayetuhumiwa kuwa mwanachama wa kundi la M23