Nyarugusu (Tanzania) : mauwaji ya mkimbizi kutoka Kongo anayetuhumiwa kuwa mwanachama wa kundi la M23

Nyarugusu (Tanzania) : mauwaji ya mkimbizi kutoka Kongo anayetuhumiwa kuwa mwanachama wa kundi la M23

Ni mwanaume ambaye aliwasili hivi karibuni katika kambi ya Nyarugusu. Aliuwawa asubuhi ya alhamisi hii. Watu wenye silaha wanaovalia sare za polisi na za kawaida walimuuwa mkimbizi huyo kutoka Kongo mjumbe wa jamii ya Banyamulenge ndani ya kambi hiyo. Alituhumiwa kwa mjibu wa vyanzo vyetu kuwa kati ya maafisa wakuu wa kundi la M23, kundi ambalo linaundwa kwa sehemu kubwa na watu wa kabila la watutsi wa Kongo. Familia ya muhanga uliwekwa chini ya ulinzi. HABARI SOS Médias Burundi

Wakimbizi ndani ya kambi ya Nyarugusu eneo la wakimbizi kutoka Kongo waliamushwa na milio ya risasi iliyodumu muda mfupi siku ya alhamisi hii.

” Watu wanaobebelea silaha ambao wanavalia sare za polisi ya Tanzania na zile za kawaida waliingia ghafla ndani ya nyumba yetu. Walimpiga risasi na akafariki papo hapo”, mke wake anaeleza huku akijawa na hofu.

Tukio hilo lilijiri katika kijiji cha 10. Muhanga alipigwa risasi mbili kifuani kwa mujibu wa mjane wake.

Washambuliaji hao, kwanza walimuuliza mkimbizi huyo kuhusu tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria, madai ambayo alipinga kabla ya kulazimishwa kutoka nje ya chumba chake, fursa ya kipekee aliyopewa ili familia yake iliweze kuuwawa.

” Kabla ya kumupiga risasi, walikuwa wakirudia kusema: ” tuonyeshe mahala ulipoficha silaha ndugu jemedali wa M23″, anakumbuka hayo mke wake. Yeye na watoto wake wamejawa na hofu. Mkuu wa familia aliuwawa mbele yao. Waliona damu ikitiririka na kuchafua nguo zao. Muili wa muhanga ulichukulia na waasi hao. Ulipelekwa na gari aina ya pick-up katika maeneo yasiojulikana.

Askali polisi wanaovalia sare

Majirani wanathibitisha kuwa waliona askali polisi wengi wanaovaa sare zao wakati wa tukio.

” Tuliona angalau gari tatu za polisi pamoja na watu wanaobebelea silaha baadhi wakivalia sare na wengine nguo za kawaida. Walikuwa wamezunguuka nyumba zote za majirani. Tulikuwa na uoga na sisi. Kwa sasa ndipo tunaelewa walichokuwa wakilenga “, wanasema.

Familia yawekwa chini ya ulinzi

Alhamisi hii mchana, ” familia ya muhanga iliwekwa chini ya ulinzi katika nyumba inayopatikana karibu na ofisi ya mkuu wa kambi, na kulindwa na polisi”, mashahidi wanaeleza.

Familia hiyo changa ilikimbia kutoka RDC kabla ya kupokelewa ndani ya kambi ya Nyarugusu mwanzoni mwa mwaka wakati Tanzania ilipopokea wimbi kubwa la wakimbizi wa Kongo wanaotoroka mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati kutokana na mapigano kati ya jeshi na waasi wa kundi la M23.

Waasi

Sababu za mauwaji hayo ya raia wa Kongo hazikujulikana rasmi. Mjane wake alipeleka mashtaka kwa polisi, ambayo ilifahamisha kuwa ” haijuwi chochote”.

Hata hivyo, vyanzo eneo hilo vinasema ” wajumbe wa idara ya ujasusi walimufuatilia tangu jumatatu hadi jumatano jioni na walichukuwa picha ya kadi yake ya kukaa kambini wakijifanya kama wafanyakazi wa mashirika ya misaada”.

Tangu ujio wake katika kambi ya Nyarugusu, mtu huyo alitajwa na majirani wake kama mtu ” anayesaidia, mzuri na aliyefunguka”, aliendelea kutuhumiwa kuwa mjumbe wa kundi la M23 na kuajiri wapiganaji ” kwa mujibu wa mmoja kati ya marafiki wake.

” Hapa, kuna watu waliompa jina la ” jenerali “. Idara ya ujasusi ilikubali daima kuwa ana jukumu ndani ya kundi la M23”, aliendelea kusema.

Polisi ilishiriki

Kuhusiana na swala la polisi ambayo inasema kuwa haijuwi chochote, wakimbizi hawakubaliani hata kidogo.

” Gari aina ya pick-up ilitoka kupitia lango kuu la polisi. Pamoja na hayo, vipi watu wa nje wanaweza kuingia ndani ya kambi hiyo kubwa na kuelekea moja kwa moja kwenye nyumba fulani ? Ni kitu kilichoandaliwa kwa umakini”, wanasema wakimbizi wa Burundi na Kongo.

Mkimbizi wa Burundi hajulikani alipo

Kabla ya kuelekea kwa muhanga, wavamiaji hao kwanza walimiteka mkimbizi kutoka Burundi. Norbert Nkundabera ni mkaazi wa kijiji cha B2.

Baada ya kutekeleza kitendo hicho, walimupeleka ndani ya gari hiyo ya Pick-up pamoja na muili wa mkimbizi huyo wa Kongo. Wakimbizi wa Burundi waliozungumza na SOS Médias Burundi wanahofia kutokea mabaya zaidi.

” Ni shahidi mmoja anayebaki, bila shaka na yeye aliuwawa tayari. Wanalaani. Wanadhani kuwa aliathiriwa kutokana na jina lake la ” Nkundabera “, linalotaka kufanana na lile la wajumbe wa jamii ya Banyamulenge. Majirani wake wanaomba uchunguzi huru ufanyike ili aweze kupatikana.

Wafanyakazi wa HCR wanaohusika na kulinda wakimbizi baada ya kushinikizwa na wakimbizi pamoja na polisi, walikubali kufanya uchunguzi ambao matokeo yake yanakosolewa sababu hawana uaminifu kwa polisi ya Tanzania.

Nyarugusu inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi laki moja na elfu 10 wakiwemo wakimbizi kutoka Kongo elfu 60.

Previous Burundi : tatizo la uhaba wa mafuta, majibu yake bado kupatikana
Next Kivu-kaskazini : watetezi wa haki za binadamu wako hatarini katika maeneo ya migogoro ya silaha