Nyarugusu (Tanzania) : wakimbizi wawili kutoka Burundi wakufa kutokana na na maji ya mvua

Nyarugusu (Tanzania) : wakimbizi wawili kutoka Burundi wakufa kutokana na na maji ya mvua

Mvua kubwa zilizonyesha katika mkoa wa Kigoma (kaskazini magharibi mwa Tanzania) ambako kunapatikana kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania zilisababisha vifo vya watu. Nyumba nyingi zilibomoka. Angalau wakimbizi wawili walifariki baada ya kusombwa na maji. HABARI SOS Médias Burundi

Mvua kubwa zilizosababisha madhara hayo zimedumu kwa wiki moja.

” Muhanga wa kwanza, ni mtoto wa miaka mitano. Alianguka katika mfereji na kupelekwa moja kwa moja na maji ya mvua katika zone 12. Muhanga wa pili ni mtu mzima mkaazi wa zone 13. Yeye alianguka katika mto Nyarugusu uliojaa na kufurika . Miwili wake uliokolewa katika eneo la makutanio ya mito Nyarugusu na Muyovozi karibu na kambi” alitoa ushahidi huo mkimbizi mmoja ambaye alizidi kuwa wawili hao wote walikuwa wakimbizi kutoka Burundi.

Mvua hizo pia ziliharibu mashamba na kubomoa nyumba na madarasa ya shule.

” Ma kumi na hata ma mia ya wakimbizi walisalia bila makaazi. Mbaya zaidi ni viongozi wa kambi kupiga marufuku kazi za kukarabati nyumba hizo. Tunajiuliza hatma ya waathiriwa hao “, vyanzo vyetu vinahakikisha na kusisitiza kuwa wanahitaji misaada ya dharura.

Katika kila msimu wa mvua, kambi ya Nyarugusu inakabiliwa na mafuriko kutokana na mahali ilipojengwa.

Kambi hiyo inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi laki moja na elfu 29 wakiwemo warundi elfu 51 wengine wanaosalia wakiwa ni kutoka Kongo.

Previous Cibitoke : waasi wa Rwanda wa kundi la FLN waripotiwa katika maeneo kadhaa ya umaa tarafani Mabayi, viongozi wachukuwa hatua ya kuwafungiana
Next Kivu-Kaskazini : zaidi ya wananchi 200 waliuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja eneo la Beni