Kivu-Kaskazini : zaidi ya wananchi 200 waliuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja eneo la Beni

Kivu-Kaskazini : zaidi ya wananchi 200 waliuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja eneo la Beni

Katika kitongoji cha Ruwenzori wilaya ya Beni mkoa wa Kivu-kaskazini (mashariki mwa DRC) , zaidi ya watu 200 waliuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja. Takwimu hizo zinatolewa na ofisi ya uratibu wa mashirika ya kiraia ya Kongo. Idadi kubwa ya wahanga waliuwawa kwa mapanga na kundi la ADF (nguvu zilizoungana kwa ajili ya demokrasia). HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa Jade Vutsapu, muhudumu katika ofisi ya uratibu wa mashirika ya kiraia nchini Kongo, tangu usiku wa tarehe 9 machi hadi 09 aprili, ” waasi wa ADF waliwauwa watu 200 katika wilaya moja ya Beni huku kitongoji cha Bashi kikiorodhesha idadi kubwa “.

” Katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia usiku wa tarehe 8 kuamkia tarehe 09 aprili , tulihesabu zaidi ya watu 200 waliouwawa kwa mapanga na waasi wa ADF. Idadi kubwa waliuwawa katika kitongoji cha Bashu, ambapo idadi iliyoorodheshwa ni zaidi ya vifo 38 waliouwawa eneo la Mukondi na 8 walikufa eneo Mwasa katika kipindi cha siku moja, lakini pia eneo la Kirindera usiku wa tarehe 11 kuamkia 12 machi watu 20 waliuwawa. Eneo la Masabanda kuelekea Oicha waliuwawa watu 21 na kuna maeneo mengine ambapo mauwaji hayo yalifanyika. Tunakasirika kuona mauwaji hayo yakitekelezwa katika maeneo ambako kuna idadi kubwa ya wanajeshi “, alibaini mwanaharakati huyo.

Jade Vutsapu anatumai kuwa mauwaji hayo yanatekelezwa katika mpango wa mauwaji ya halaiki yanayolenga wananchi wa wilaya ya Beni.

Anaomba serikali kutathimini upya mkakati wake wa amani na usalama katika eneo hilo.

Previous Nyarugusu (Tanzania) : wakimbizi wawili kutoka Burundi wakufa kutokana na na maji ya mvua
Next Bujumbura : kongamano lisilokuwa la kawaida la chama cha CNL lasimamishwa kwa kosa "la tahajia"