Bujumbura : kongamano lisilokuwa la kawaida la chama cha CNL lasimamishwa kwa kosa “la tahajia”

Bujumbura : kongamano lisilokuwa la kawaida la chama cha CNL lasimamishwa kwa kosa “la tahajia”

Kutokana na kosa katika kuandika barua inayotumwa kwa waziri wa mambo ya ndani, chama cha upinzani cha CNL kilizuiliwa kuandaa kongamano lake kuu lililokuwa limepangwa kufanyika mchana wa ijumaa tarehe 14 aprili. HABARI SOS Médias Burundi

Katibu mtendaji wa chama cha CNL anafahamisha kuwa ” tulipewa taarifa kupitia simu alhamisi usiku kuwa kongamano halitafanyika kwa sababu ya kosa la kimandishi ndani ya barua iliyotumwa kwa waziri wa mambo ya ndani”.

Tulivunjika moyo katika chama hiki cha upinzani ambacho mara nyingi hakiruhusiwi kutekeleza programu zake kama ilivyopangwa.

Simon Bizimungu katibu mtendaji wa chama hicho, anaomba waziri husika kushirikiana na vyama vya kisiasa na kutoa majibu kwa barua za vyama kwa wakati.

” Hali hiyo itasaidia kujiepusha na matatizo ya dakika ya mwisho” alieleza.

Tarehe 19 februari iliyopita, waziri wa Burundi wa mambo ya ndani Martin Niteretse alipiga marufuku sherehe za maadhimisho ya mwaka wa nne wa chama cha CNL akidai kuwa hali ya mvutano ndani ya chama hicho inaweza kuvuruga usalama katika mji mkuu wa kibiashara wa Bujumbura na kwenye barabara zinazounganisha mji huo na mikoa mbali mbali kabla ya badaye kuruhusu sherehe hizo kufanyika tarehe 12 machi.

Katika maeneo kadhaa, wafuasi wa CNL mara nyingi hunyanyaswa, kuuwawa na kuteswa lakini pia wanafungwa kinyume cha sheria. Wanaofanya vitendo hivyo, ni wafuasi wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD, wajumbe wa idara ya upelelezi, askali polisi pamoja pia na viongozi wa ndani na askali jeshi kwa kiwango kidogo kulingana na mashirika ya kutetea haki za binadamu na vyanzo vya SOS Médias Burundi.

Kwa mjibu wa Carina Tertsakian mtafiti mshirika wa IDHB ( Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Burundi), kuna tofauti kubwa kati ya ahadi za rais Neva na vitendo kuhusu swala la kuheshimu haki za binadamu “.

Previous Kivu-Kaskazini : zaidi ya wananchi 200 waliuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja eneo la Beni
Next RDC (Ituri) : angalau wananchi 40 waliuwawa na waasi wa CODECO