Gihanga : bibi kizee wa zaidi ya miaka sabini auwawa

Gihanga : bibi kizee wa zaidi ya miaka sabini auwawa

Mwanamke mwenye wa miaka 75 alikatwa kichwa na watu wasiojulikana bado katika kijiji cha Rugunga tarafa ya Gihanga mkoa wa Bubanza (magharibi mwa Burundi). Polisi tayari iliwakamata watuhumiwa watatu. HABARI SOS Medias Burundi

Janga hilo lilitokea usiku wa jumanne tarehe 12 kuamkia jumatano 13 septemba katika kijiji cha Rugunga. Jacqueline Nahishakiye mwenye umri wa miaka 75 aliuwawa akiwa nyumbani kwake.

” Maiti yake ilikuwa ikilala ndani ya damu huku kichwa kikiwa kilikatwa kwa kutumia panga”, alitoa ushahidi huo jirani.

Mkuu wa kijiji cha Rugunga, Célestin Rivugo akizungumzia na SOS Médias Burundi alithibitisha habari hizo na kuzidi kusema kuwa mauwaji hayo yalisababishwa na mizozo ya ardhi.

Kifo chake kilitokea siku moja baada ya kuzuru ardhi anazomiliki.

Uvumi mwingi unahusisha baadhi ya wajumbe wa familia yake kama watu walioandaa mauwaji hayo.

Ndugu wa muhanga ambaye walikuwa hawaelewani kwa muda mrefu kulingana na mashahidi katika kijiji cha Rugunga kwa sasa anazuiliwa katika gereza la tarafa ya Gihanga.

Watu wa karibu na muhanga wanaomba wapelekwe mahakama haraka waliohusika na mauwaji hayo.

Previous Burundi : bei ya tiketi ya usafiri yapanda
Next Nyarugusu (Tanzania) : askali wanne wasimamishwa kwa tuhuma za jaribio la wizi