Burundi : bei ya tiketi ya usafiri yapanda

Burundi : bei ya tiketi ya usafiri yapanda

Waziri wa biashara alitangaza jumatano hii bei mpya na nauli ya usafiri ndani ya mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura na katika ya mikoa. Bei ya tiketi ndani basi mjini Bujumbura popote pale unapotoka na kuelekea kati kati mwa mji ilipandishwa franka 50 sarafu za Burundi. Kati kati mwa nchi nauli itapanda kwa franka 500. HABARI SOS Médias Burundi

Waziri Marie Chantal Nijimbere alifahamisha kupitia tangazo kuwa bei ya nauli za usafiri ilipandishwa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ya gari tangu jumatatu hii.

Wakaazi wa jiji la Bujumbura walibaini kuwa walitaraji ongezeko hilo la bei ya tiketi litatokea.

” Bila shaka na bei ya vyakula na bidhaa zingine mahitajio muhimu zitapanda”. wanalaani wakaazi wengine ambao wanazidi kuwa walitupiliwa “.

Wengine wanasema kuwa hawaelewi malengo ya serikali. Wafanyakazi wa umma wanasema kuwa serikali inalenga kukusanya pesa iliyotumia katika kutekeleza sera ya kusawazisha mishahara iliyoanza kutelelezwa tangu julai iliyopita”.

” Bei ya bidhaa muhimu itapanda pia kwa mkondo huo”, wanalaani wafanyakazi wa serikali.

Bei ya tiketi ya usafiri ilipanda mara ya mwisho katika mwezi julai iliyopita.

Hatua hiyo ilisababisha bei ya bidhaa zingine kama sukari, simenti na vinywaji kupanda licha ya kuendelea kuadimika kwenye soko nchini Burundi.

Previous DRC (Uvira) wakimbizi wawili wenye asili ya Burundi wakamatwa kwa jaribio la mauwaji
Next Gihanga : bibi kizee wa zaidi ya miaka sabini auwawa