DRC (Uvira) wakimbizi wawili wenye asili ya Burundi wakamatwa kwa jaribio la mauwaji

DRC (Uvira) wakimbizi wawili wenye asili ya Burundi wakamatwa kwa jaribio la mauwaji

Wakimbizi wenye asili ya Burundi katika kambi ya muda ya Kavimvira mjini Uvira katika mkoa wa Kivu kusini mashariki mwa DRC walikamatwa kwa tuhuma za jaribio la mauwaji. Mmoja anafuatiliwa kwa jaribio la kumuuwa mvuvi mmoja wakati wa pili akiwa alijaribu kumumalizia maisha mlinzi wa kambi. Wawili hao raia wa Burundi wanazuiliwa ndani ya gereza la polisi mjini Uvira. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na Kiza Tiniko, kiongozi wa vijana eneo la Kavimvira, wakimbizi hao wawili walikamatwa jumatatu tarehe 11 septemba 2023.

” Kijana mkimbizi mwenye uraia wa Burundi kwa jina la Mugisha Justin mkaazi wa kambi ya Kavimvira alijaribu kumumalizia maisha kijana mvuvi mwenye uraia wa Kongo kwa jina la Matabishi Saleh ilikuwa majira ya saa 6 na dakika 15 katika kata ya Kavimvira barabara ya Lac. Vijana wakaazi wa kata hiyo waliingilia kati [….], alisema.

Kwa mjibu wake, kisu ambacho mkimbizi huyo wa Burundi alitaka kutumia kilikamatwa .

Mkimbizi mwingine anazuiliwa jela kwa tuhuma za jaribio ya kumuuwa mlinzi wa kambi ya muda ya Kavimvira.

Habari hizo zinathibishwa na mfanyakazi wa tume ya kitaifa kwa ajili ya wakimbizi mjini Uvira. Anahakikisha kuwa uchunguzi ulianzishwa na polisi eneo hilo.

Kambi ya muda ya Kavimvira inawapa hifadhi zaidi ya watu 3000 wenye asili ya Burundi.

Previous Burundi : bei ya mafuta ya gari yapanda kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili
Next Burundi : bei ya tiketi ya usafiri yapanda