Nyarugusu (Tanzania) : askali wanne wasimamishwa kwa tuhuma za jaribio la wizi

Nyarugusu (Tanzania) : askali wanne wasimamishwa kwa tuhuma za jaribio la wizi

Askali polisi walifumaniwa wakifanya wizi ndani ya makaazi ya mfanyabiashara mmoja katika kambi ya Nyarugusu. Polisi hao walikamatwa pamoja na walinzi wa kawaida watatu wa kambi. Wakimbizi wanaomba adhabu kali zichukuliwe dhidi yao. HABARI SOS Médias Burundi

Ijumaa iliyopita, majira ya saa 2 usiku, watu saba wanaovalia nguo za kawaida waliwasili katika makaazi ya mfanyabiashara wa kijiji cha 9 katika kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania.

” Wakati walipogonga kwenye mlango wa bati, mfanyabiashara huyo kwa jina la ” Gasongo” alifungua akifikiria kuwa ni wateja waliochelewa ambao wanaingia kununua pombe. Lakini hali ilikwenda kinyume.

” Walinyanyua silaha na kuilekeza kwake, na kumpa amri ya kuwapa pesa yote aliyokuwa nayo. Alijibu kuwa hana pesa, na kwamba aliagiza bidhaa kwa ajili ya duka lake. Lakini alikuwa tayari ameona sura zao “, majirani walieleza.

Wezi hawakuishia hapo.

” Waliomba shilingi 400 000 ili wasiwamalizie maisha. Muhanga aliwaomba msamaha na kuwaambia kuwa alipata nusu. Wavamiaji hao walikubali na kumuacha aingie ndani ya nyumba ili kuchukuwa pesa hiyo “, majirani waliendelea kueleza.

Mara baada ya kuingia chumbani kwake, ” Gasongo “alimpigia simu kamanda wa polisi inayofanya ulinzi wa kambi pamoja na walinzi wa kawaida. Watu hao hawakuchelewa kuingilia kati.

” Askali polisi, walinzi na baadhi ya viongozi wa wakimbizi walielekea katika kijiji cha 9 kwa makaazi ya Gasongo na kuzunguuka uwa wake. Purukushani nusra ifanyike, lakini wezi hao walijisalimisha. Wote saba walifungwa pingu na kupandishwa gari la polisi”, mashahidi wanaeleza.

Kwa sasa , wanazuliwa katika jela la polisi. Wakimbizi wanaomba wapewe adhabu kali.

” Hatimaye tumefahamu kuwa ni askali polisi wanaotuiba na kutumalizia maisha. Kwa hiyo, wale waliofumaniwa wapewe adhabu kali . Pia tunahofia maisha ya mfanyabiashara huyo, wanaweza kulipiza kisasi” wanamtetea.

Mwanzoni mwa mwezi huu, katibu wa kudumu anayehusika na maswala ya wakimbizi katika wizara ya mambo ya ndani, Sudi Mwakibasi, alihakikisha kuwa maovu yanafanyika dhidi ya wakimbizi wa Burundi mara kadhaa, polisi ikihusika na aliahidi kuwa hali hiyo itabadilika, na kutoa matumaini kuwa wanaofanya ukatili huo wataadhibiwa.

Wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu ambako Mwakibasi alitoa hutba hiyo wanaomba vitendo viweze kufuata maneno .

Nyarugusu inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi 110.000 wakiwemo warundi zaidi ya elfu 50 huku wengine wakiwa raia wa Kongo.

Previous Gihanga : bibi kizee wa zaidi ya miaka sabini auwawa
Next Mahama (Rwanda) : ukosefu wa mara kwa mara wa gesi kwa ajili ya kupika chakula