Kuhusu-Bunyoni: mahakama kuu imeanza uchunguzi dhidi ya Bunyoni
Korti kuu ya jamuhuri ya Burundi imeamuru kufungua uchunguzi kuhusu kushughulikia kisheria kesi dhidi ya Bunyoni. Mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri amefahamisha hayo katika tangazo lake jumapili hii. Hata hivyo, tume ya kitaifa ya haki za binadamu haikueleza mahala anapozuiliwa aliyekuwa waziri mkuu mwenye nguvu. HABARI SOS Médias Burundi
Tamko lilolotolewa na mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri linafahamisha kuwa waziri mkuu wa zamani Alain Guillaume Bunyoni anashikiliwa na polisi ya Burundi.
” Alikamatwa akiwa eneo la Nyamuzi, kijiji cha Mubone tarafani Kabezi katika mkoa wa Bujumbura ( magharibi mwa Burundi ) tarehe 21 aprili 2023″, linasema tangazo lililosainiwa na Sylvestre Nyandwi.
Kwa mjibu wa mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri, taasisi za Burundi zilianza rasmi kumutafuta Bunyoni tarehe 17 aprili baada ya polisi kutomukuta nyumbani kwake wakati wa msako ulioruhusiwa na ofisi yake.
” Jemedali wa polisi Alain Guillaume Bunyoni kwa sasa yuko mikononi mwa polisi. Matokeo ya msako na ushahidi mwingine utatathminiwa hivi karibuni na kuwekwa mahala pake, kwa kuzingatia utaratibu wa kushughulikia makosa”, tangazo hilo linamalizia.
Kama CNIDH ( tume huru ya kitaifa ya haki za binadamu), mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri hakufahamisha pia mahala anakozuiliwa waziri mkuu wa zamani.
Lakini vyanzo vya karibu na faili hiyo vimethibitishia SOS Médias Burundi kuwa anazuiliwa katika gereza la SNR ( idara ya kitaifa ya ujasusi) ndani ya jiji la kibiashara la Bujumbura.
” Hajapata haki ya kupewa wakili. Ni kiongozi wa CNIDH aliyekwenda nyumbani kwake kumuletea nguo za kubadilisha”, vyanzo vyetu vinasema.
Alain Guillaume Bunyoni analengwa na vikwazo vya Marekani. Nchi hiyo yenye nguvu duniani inamutuhumu kuhusika na visa vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Burundi.
” Marekani haiwezi kuomba serikali ya Burundi ashughulikiwe na mahakama za kimataifa kwa sababu, marekani ilimuzuia tu kuwasili kwenye ardhi ya marekani”, alitoa tathmini hiyo mwakilishi wa shirika la kiraia aliyetoroka nchi.
Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, ” mazungumzo yanaendelea ili adhabu ya Bunyoni iweze kupunguzwa”. Baadhi ya vigogo wa chama madarakani, viongozi tawala, wanajeshi wa vyeo vya juu kutoka kundi la zamani la waasi wa ki hutu la CNDD-FDD wanataka Bunyoni aweze kuadhibiwa vikali ” ili kuepusha mgawanyiko ndani ya chama cha CNDD-FDD”.
About author
You might also like
Bujumbura: Rais Neva anataka kuning’inia
Jedwali la pande zote la washirika wa maendeleo na wawekezaji wa kigeni limefanyika tangu Alhamisi mjini Bujumbura, mji wa kibiashara wa Burundi. Lengo ni kukusanya fedha kwa ajili ya utekelezaji
Burundi : ni mapema kubainika wazi madhambi ya Bunyoni
Mahakama kuu ya Burundi alhamisi hii ilifahamisha kuwa mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri anaendelea kutafuta mashtaka mapya dhidi ya Bunyoni. Msemaji wa mahakama kuu na ofisi ya mwendeshamashtaka mkuu aliyefahamisha hayo,
Uvira (DRC): mfanyakazi wa ngono mwenye asili ya Burundi auawa
Esta. N aliuawa Septemba 1 katika chumba cha hoteli huko Uvira. Iko katika jimbo la Kivu Kusini mashariki mwa DRC. Muhusika wa mauaji hayo angekuwa mteja wake ambaye alitokomea porini.