Kuhusu-Bunyoni : kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia abadilishwa

Kuhusu-Bunyoni : kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia abadilishwa

Ni wizara ya mambo ya ndani na usalama iliyochukuwa uamzi huo. Kanali wa polisi Désiré Uwamahoro aliyekuwa kiongozi wa kikosi kinachokosolewa cha kutuliza ghasia (BAE) alirejelewa na kanali mwingine. Jonathan Sindayihebura hadi jumatatu tarehe 24 aprili alikuwa akifanya kazi ndani ya kikosi cha API (kikosi cha kuwalinda viongozi). HABARI SOS Médias Burundi

Kanali wa polisi Désiré Uwamahoro anazuiliwa katika jela kuu la Murembwe mkoani Rumonge ( kusini magharibi mwa Burundi) tangu aprili 21 iliyopita.

Alitumwa katika gereza hilo baada ya wiki moja akizuiliwa ndani ya gereza la SNR ( idara ya ujasusi nchini Burundi) katika mji mkuu wa kiuchumi Bujumbura kutokana na kesi dhidi ya Bunyoni, vyanzo vinasema.

” Rais alikuwa ameamuru kuwa baada ya kufutwa kazi, waziri mkuu wa zamani asipewe walinzi. Baada ya kutoka ziarani nchini Marekani, rais aligundua kuwa maamuzi yake hayakutekelezwa kikamilifu. Alionyesha hasira dhidi ya waziri mkuu katika mkutano ndani ya ikulu. Baada ya matakwa yake kutimia, Désiré Uwamahoro kwa ushirikiano na maafisa wa cheo katika polisi, walituma askali polisi kwenye ngome inayopatikana karibu na makaazi ya Bunyoni (kusini mwa jiji la Bujumbura). Hakika walikuwa na ujumbe wa kulinda usalama wa Bunyoni lakini kisheria, walidai kuwa wanafanya ulinzi wa eneo hilo” vyanzo vya karibu na faili vinafahamisha.

Kanali Uwamahoro aliyerejelewa kwenye wadhifa wa kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia, mwezi novemba 2016, alifutwa kazi kwa kosa la kufanya biashara haramu ya dhahabu kabla ya kupewa heshima na tuzo na hayati Pierre Nkurunziza.

Yeye na kikosi chake, wanatuhumiwa kufanya maovu mengi na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika kata ambazo zilishudia mandamano dhidi ya muhula wa kutatanisha wa hayati Pierre Nkurunziza mwaka wa 2015 na miaka iliyofuata katika jiji la kibiashara la Bujumbura na hususan katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Bujumbura.

Sheria ya waziri wa mambo ya ndani na usalama inayomuteuwa mrithi wake kamanda mpya wa kikosi cha kutuliza ghasia ilishuhudiwa na SOS Médias Burundi jumanne asubuhi. Vyanzo katika ofisi kuu ya polisi vilithibitisha sheria hiyo.

Kanali wa polisi Désiré Uwamahoro na mrithi wake wote wawili ni kutoka kundi la zamani la waasi wa kihutu wa CNDD mzizi wa CNDD-FDD chama tawala kwa sasa tangu 2005 kutokana na makubaliano ya amani na maridhiano ya Arusha ya mwezi agosti 2000.

Kikosi cha kutuliza ghasia ni moja kati ya vikosi maluum vya PNB ( polisi ya Burundi). Kikosi hicho kinaundwa na wafuasi wa chama waliochaguwa kukabiliana na waliopinga muhula mwingine wa hayati rais Pierre Nkurunziza katika mwaka wa 2015. Kikosi hicho kilianzishwa mwaka huo.

Kwa mjibu wa sheria ya Burundi, anatakiwa kushughulikiwa na mahakama ya rufaa kama afisa wa cheo. Kutokana na hali hiyo, angetakiwa kufungwa katika tarafa ya Mukaza ( makao makuu ya kiuchumi ya Bujumbura) ambako kikosi chake kinafanyia kazi.

Akimalizia miezi sita jela, atafutwa mara moja ndani ya PNB kulingana na sheria inayotekelezwa ndani ya nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki.

Hadi sasa, mashtaka dhidi yake bado hayajawekwa wazi na vyombo vya sheria vya Burundi.

Lakini jumatano iliyopita, waziri wa Burundi wa mambo ya ndani na usalama aliwambia wandishi wa habari kuwa “[…] Désiré Uwamahoro anafuatiliwa na mahakama kuu ya jamuhuri”. Martin Niteretse alijizuia kutoa maelezo kamili kuhusiana na faili hiyo.

Previous Kuhusu-Bunyoni: mahakama kuu imeanza uchunguzi dhidi ya Bunyoni
Next Burundi: utawala wa rais Ndayishimiye unafanya mauwaji kama ule wa mtangulizi wake Nkurunziza