Mahama (Rwanda) : ukosefu wa mara kwa mara wa gesi kwa ajili ya kupika chakula
Wakimbizi katika kambi ya Mahama nchini Rwanda wanalaani hali ya mara kwa mara ya kukosa gesi ya kupika chakula. Kila mwezi gesi inachelewa kwa angalau wiki mbili. Hali hiyo inazidisha umasikini unaowakabili wakimbizi wenye asili ya Burundi na Kongo ndani ya kambi hiyo. Wanaomba vituo vya kugawa gesi hiyo viongezwe badala ya kimoja tu ambacho kinafanya kazi kwa sasa. HABARI SOS Médias Burundi
Wiki hii, wakimbizi ndani ya kambi ya Mahama iliyopo mashariki mwa Rwanda wanapata msaada wa gesi ya kupika chakula ambao wangepewa mwishoni mwa mwezi agosti iliyopita.
” Ni hali ya kukosolewa, ni kama vile tangu mwishoni mwa mwezi agosti hadi siku hii , hakuna nishati kwa ajili ya kupika chakula. Hali hiyo inatupelekea mara kadhaa kulala bila kula kutokana na uhaba wa gesi ya kupikia chakula “, wanaeleza wakimbizi kutoka Burundi.
Katika mkoa wa mashariki ambako kunapatikana kambi hiyo, watetezi wa mazingira ni wakali kuhusiana na swala la kukata miti kwa ajili ya kupikia chakula.
” Mkimbizi aliyekamatwa akiwa na kuuni anapewa adhabu ya kifungo. Hakuna anayekwenda msituni kutafuta kuuni za kupikia”, wanalaani wakimbizi.
Ili kukabiliana na hali hiyo, ” wakimbizi wanatumia miti ya parachichi , nguo zilizochanika, nawe na kitu chochote kinachoweza kupasha chungu”, wanasema wakimbizi.
Changamoto hiyo ya ukosefu wa gesi ya kupikia ilianza kushuhudiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Kituo kimoja peke cha kugawa gesi hiyo ndicho kinafanya kazi. Wakimbizi wanaomba viwepo vituo vingi vya kusambaza gesi.
Kwa mujibu wa wahudumu wa HCR, tatizo hilo litapata majibu.
” Mjasiliamali mwingine alipata soko na shughuli za ujenzi wa kituo kingine zinaendelea katika Kijiji cha 11, eneo la Mahama II . Kwa njia hiyo tutapunguza milolongo mirefu ya wakimbizi wanaosubiri na hivyo kuwapunguzia uzito wakimbizi hao ambao hawana njia mbadala ya kuweza kupika chakula chao”, wanahakikisha .
Wakimbizi wanaridhia lakini bado wanasalia na dukuduku.
” Acheni tusubiri tutaona. Ni kweli shughuli za ujenzi zinaelekea kukamilika , lakini bado tuna wasi wasi. Wanakisia kuwa HCR itawapatia pesa ili kujinunulia wenyewe mitungi ya gesi kwa wajasilimali hao. Hapo tuna uhakika kuwa wakimbizi hao watatumia pesa hiyo kwa ajili ya manunuzi mengine, ikizingatiwa kuwa umasikini umekithiri hapa. Ni budi wasimamizi walitathimini swala hilo kwa urefu ili wasituingizi katika makosa”, wakimbizi wa Burundi wanasema.
Wakimbizi hao wanaomba HCR na PAM (WFP) pamoja na wizara inayohusika nao, MINEMA kuongeza msaada wa chakula na pesa kwa sababu, bei masokoni ilipanda kwa kiwango kikubwa, mara mbili hadi mara tatu kwa baadhi ya bidhaa mahitajio muhimu.
Ofisi ya Rwanda kwa ajili ya maendeleo, RDB hivi karibuni, ilitangaza kuwa hali ya sarafu yao kupoteza thamani , itaathiri maisha ya kila siku ya wananchi wa kima cha chini. Na wakimbizi wakiwa mstari wa mbele kwa tishio hilo.
Kambi ya Mahama inazidi kupanuka haraka sababu inaendelea kuwapokea wakimbizi kutoka mkoa wa Kivu kaskazini hali inayomanisha kuwa kuna uhitaji wa mashirika mengi ya misaada yaliyokuwa yalisimamisha tangu mwanzoni mwa zoezi la kuwarejesha makwao kwa hiari wakimbizi wa Burundi katika mwaka wa 2020.
Kambi hiyo kwa sasa inawapa hifadhi watu zaidi ya elfu 55.000 idadi kubwa ikiwa wakimbizi kutoka Burundi.