Bujumbura : uimarishwaji wa usalama mbele ya RTNB wasababisha wasi wasi

Bujumbura : uimarishwaji wa usalama mbele ya RTNB wasababisha wasi wasi

Wafanyakazi wa radio na televisheni ya Burin di (RTNB) kituo cha matangazo cha serikali, walishituka kuona ijumaa asubuhi, kikosi kikubwa cha usalama pamoja na uwepo wa mbwa wa polisi kwenye lango la kuingilia. Ulinzi katika viingilio vinavyolindwa na askali jeshi wa kikosi maluum cha kulinda taasisi (BSPI) uliimarishwa pia. HABARI SOS Médias Burundi

Wafanyakazi wa kituo hicho cha matangazo cha serikali kinachopatikana katika kata ya kabondo kwenye umbali wa kilometa moja kutoka makao makuu ya Bujumbura ( mji mkuu wa kibiashara) walipata tabu kuvuka baadhi ya vizuizi ili kuingia ndani.

Wafanyakazi waliozungumza na SOS Medias Burundi walifahamisha kuwa walilazimika kuonyesha kadi inayowapa idhini ya kuingia ndani ya RTNB ili kuvuka kiuziwizi za kwanza.

Na kuongeza kuwa gari ya kituo hicho au ya binafsi hazikuruhusiwa kuingia ndani ya kituo hicho bila kukaguliwa na mbwa.

” Tangu miaka zaidi ya ishirini nikihudumu ndani ya RTNB, sijawahi kuona mbwa wa kipolisi kwenye lango. Harafu nilikuwa sijawahi kusikia tetesi zinazohusisha wafanyakazi wa kituo hicho cha matangazo cha serikali”, alilalamika mfanyakazi huyo wa kituo cha serikali.

” Hali tunayoona si ya kawaida”, alitoa ushuhuda huo mfanyakazi mwingine ijumaa asubuhi.

Jaribio la kawaida ?

Kwa mjibu wa afisa wa jeshi wa kikosi cha BSPI anayefanyia katika ikulu ya rais , lilikuwa ni zoezi la kawaida na kuzoweza mbwa wapya walioagizwa hivi karibuni kutoka Afrika ya kusini.

Anahakikisha kuwa ” tuliimarisha usalama ndani ya RTNB”. Lakini hakueleza sababu.

” Hakuna sababu zilizotolewa ” aliambia SOS Médias Burundi mwandishi wa RTNB.

Hakuna uwezekano wa shambulio

Kulingana na vyanzo katika idara ya usalama, viongozi wa Burundi wanahofia shambulio baada ya shambulio lililodaiwa kufanywa na waasi wa Red Tabara* katika eneo la Buringa ( mkoa wa Bubanza magharibi) usiku wa tarehe 2 kuamkia 3 septemba iliyopita.

” Kuna habari zinazosambaa kuhusu uwepo wa kundi la waasi linaloweza kutekeleza shambulio kwenye ardhi ya Burundi wakati wowote. Kundi hilo linaongozwa na raia wa Kabila la bahutu na idadi kubwa ya wapiganaji wake wanapiga kambi nchini DRC. Dalili zote zikiwa za tahadhari na hali ya kuvunjika moyo ikiendelea kuingia katika mioyo ya watu , ni kawaida kwa rais na watu wake wa karibu kuchukuwa tahadhari”, amebaini muangalizi wa ndani wa karibu na chama cha CNDD-FDD chama tawala.

Kulingana na mwandishi wa habari wa Burundi anayepata habari nyingi kutoka chama tawala , rais Neva hana uaminifu na mtu yoyote mnano siku hizi.

” kwa sasa , rais anatenda mwenyewe . Ni kama vile hata ma waziri hawana kazi. Ndio sababu unamuona rais akifanya siku nyingi akilalamika pasina kuonekana vitendo ” anafahamisha.

Aliendelea kusema :” hali ya sasa ni tofauti na wakati wa Nkurunziza. Ni watu wachache wanaoweza kujitolea muhanga kwa manfaa ya rais Neva. Anafahamu hilo na ni lazima aweze kuimarisha ulinzi wake”.

Kwa mjibu wa wakaazi wa jiji la kibiashara, zoezi linalotajwa kama la kawaida, la uchunguzi wa kadi za uraia unafanyika katika daraza za Bujumbura tangu alhamisi jioni.

Tangu jaribio la mapinduzi lililofeli tarehe 13 mei mwaka 2015, magari ya kazi ndio yanaruhusiwa peke kuingia ndani ya majengo ya RTNB.

Gari za watu binafsi zinapewa ruhsa maluum ili ziweza kuingia ndani ya kituo hicho cha matangazo cha serikali.

Previous Mahama (Rwanda) : ukosefu wa mara kwa mara wa gesi kwa ajili ya kupika chakula
Next Burundi : viongozi wa Burundi wapiga marufuku kongamano la kimataifa la akinamama waumini wa kikristu