Burundi : viongozi wa Burundi wapiga marufuku kongamano la kimataifa la akinamama waumini wa kikristu

Burundi : viongozi wa Burundi wapiga marufuku kongamano la kimataifa la akinamama waumini wa kikristu

Viongozi wa Burundi alhamisi hii walifahamisha kuwa kongamano la kimataifa la kikristu la akinamama halitafanyika. Kongamano hilo liliandaliwa na shirika linaloongozwa na mchungaji kutoka Rwanda. Waziri wa mambo ya ndani na usalama alisema ” walitumia kinyume ruhsa”. HABARI SOS Médias Burundi

Tukio hilo lingewapokea washiriki zaidi ya elfu nne kutoka ma bara tofauti kwa mjibu wa waandaji ambao wanasema kuwa bado wana matumaini viongozi wataruhusu kongamano hilo lifanyike. Kongamano hilo lingefanyika kusini mwa jiji la kibiashara la Bujumbura tarehe 15 hadi 17 septemba 2023.

Katika barua ya kusimamisha maandalizi ya kongamano hilo ambayo SOS Médias Burundi ilipata, waziri wa Burundi wa mambo ya ndani na usalama Martin Niteretse anawatuhumu waandaji wa kongamano hilo kutumia kinyume ruhsa waliopewa.

“[….], tulipata taarifa kuwa mulitumia ruhsa hiyo vibaya, jambo ambalo ni kinyume na yale mulioandika katika barua yenu” alituhumu waziri Niteretse.

Sababu za ukweli

Mchungaji Mignonne Kabera ambaye angetoa mafunzo kwa kipindi cha siku tatu mjini Bujumbura anafuatiliwa na raia wa Burundi na Rwanda wakiwa ndani ya nchi zao hata pia na wananchi wa mataifa hayo mawili ndugu ya eneo la maziwa makuu ya Afrika wanaoishi nje ya nchi. Kabla ya kuwasili kwake ndani ya mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi alhamisi hii, wandaaji waliomba watu wenye nia ya kushiriki kuunga mkono kituo kwa kuchangia pesa. Akaunti mbili zilifunguliwa kwa malengo hilo : moja ya dola na nyingine ya sarafu za Burundi.

” Watu wengi nchini Burundi, Rwanda na ugenini waliunga mkono shughuli hiyo. Waliweka vitita vikubwa vya pesa kwenye akaunti hizo. Hiyo ndio sababu peke iliyopelekea viongozi wa Burundi kupiga marufuku shughuli hiyo”, alibaini muamini wa dhehebu la karibu na waandaji wa kituo hilo. Haijabainika wazi iwapo waziri wa mambo ya ndani ya usalama atakwenda hadi ” kuwalazimisha kurudisha pesa iliwekwa kwenye akaunti hizo mbili”.

” Viongozi wetu wana matatizo. Vipi unaweza kuzuiwa tukio hilo kufanyika katika nchi ambayo inahitaji pesa za kigeni na wageni wakati tukio hilo lingewaleta pamoja watu wengi. Na pia ni njia ya kutangaza Burundi . Hivi karibuni hata mke wa rais wa Rwanda alihudhuria kongamano kama hilo lililofanyika mjini Kigali ” alifahamisha muangalizi wa Burundi anayeishi nje ya nchi .

Washiriki wengi wenye uraia wa Burundi na wageni, wanaoishi nje ya taifa hilo dogo la Afrika mashariki tayari walikuwa wamewasili mjini Bujumbura kwa ajili ya kuhudhuria kongamano hilo la ” Connect Afrika Conference 2023″.

Waliozungumza na SOS Médias Burundi wanasema kuwa ” wamechanganyikiwa “.

Mwezi agosti iliyopita, angalau watu elfu 5 washiriki kutoka pembe nne za dunia walijikuta katika mji mkuu wa Kigali Rwanda kuhudhuria kongamano la aina hiyo.

Mke wa rais wa Rwanda Jeannette Kagame alikuwa miongoni mwa washiriki katika kongamano hilo ambapo mioyo mingi ilijengengwa na ushuhuda usiokuwa wa kawaida ambao ulitolewa, kwa mujibu wa mjumbe wa moja kati ya madhehebu ya kikristu yenye waumini wengi ndani ya eneo la maziwa makuu ya Afrika .

Previous Bujumbura : uimarishwaji wa usalama mbele ya RTNB wasababisha wasi wasi
Next Burundi : bei ya mbolea ya kizungu yapandishwa