Burundi : bei ya mbolea ya kizungu yapandishwa

Burundi : bei ya mbolea ya kizungu yapandishwa

Serikali ya Burundi ilipandisha bei ya mbolea ya kizungu. Hayo yalifahamishwa na waziri wa kilimo katika mkutano na wandishi wa habari alhamisi tarehe 14 septemba iliyopita. Sanctus Niragira alisisitiza kuwa kiwanda cha FOMI (kinachotengeneza mbolea) hakina changamoto yoyote kuhusiana na kuweka tayari mbolea na kwa wakati. Hata hivyo, wiki iliyopita, meneja mkuu wa FOMI alihakikisha kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na matatizo ya kiufundi ili kuweza kutengeneza mbolea ya kiwango cha kutosha na wakati inaofaa. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mujibu wa waziri Sanctus Niragira, wakulima wanatakiwa kutekeleza bei mpya ya mbolea iliyopangwa.

Mfuko wa kilo 25 wa mbole aina ya Urée utanunuliwa 91.965 sarafu za Burundi “. Serikali itatoa 58965 huku mkulima akitoa 33.000 sarafu za Burundi zinazosalia . Mfuko wa mbolea aina ya FOMI BAGARA utanunuliwa 77. 473 sarafu za Burundi zikiwemo franka 49.473 zitazofadhiliwa na serikali dhidi ya franka 28.000 ambazo zitatolewa na mkulima. Mifuko miwili ya mbolea maarufu Dolomie ya kilo 25 ( kg 50) itanunuliwa franka 19000 zikiwemo franka elfu 14 ambazo zitatolewa na serikali huku upande wa mkulima akitakiwa kulipa elfu 5 , kama alovyoendelea kusema waziri.

Waziri huyo aliendelea kuhakikisha kuwa mfamo wa serikali wa kulipia sehemu ya bei ya mbolea ili kuwarahisishia wakulima utaandelezwa.

Ama kuhusu iwapo hapatakuwa kuchelewesha mbolea, waziri Sanctus Niragira anatuliza huku akihakikisha kuwa mbolea inayohitajika itatolewa kwa wakati.

Na kuhusu mbolea ya kemikali ilioahidiwa na Urusi, Sanctus Niragira alionekana kama mtu ambaye hana taarifa hizo.

” ahadi hiyo ilitolewa hivi karibuni ” alifahamisha wakati ambapo msaada huo unaozungumziwa uliahidiwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Previous Burundi : viongozi wa Burundi wapiga marufuku kongamano la kimataifa la akinamama waumini wa kikristu
Next Bujumbura : kazi zavurugika kutokana na umeme unaokatika mara kwa mara