Bujumbura : kazi zavurugika kutokana na umeme unaokatika mara kwa mara

Bujumbura : kazi zavurugika kutokana na umeme unaokatika mara kwa mara

Hali ya umeme kukatika mara kwa mara inaripotiwa katika mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura. Wakaazi wanalalamika huku wafanyabiashara wanaoendesha shughuli za kibiashara wakidai kupata hasara kubwa. Mamlaka ya maji na umeme Regideso bad o haijatoa maelezo. HABARI SOS Medias Burundi

Ni wengi wanaolalamika kutokana na hali hiyo ya umeme kukatika mara kwa mara ndani ya mji wa Bujumbura.

” Tunalazimika kulipa franka elfu moja za ziada kwenye gharama ya kushevu nywele. Ni pesa nyingi wakati uchumi wa nchi ukiwa mbaya “, aliambia SOS Medias Burundi akiwa na hasira mwanamke mmoja aliyekuwa akitoka katika chumba cha kutengeneza nywele za wanawake.

Wanaofanya kazi ya kuchevu nywele wanasema kuwa hali hiyo huwaletea shida na wateja wao sababu hawaelewi tatizo la kutumia mafuta ya gari. Ni bidhaa inayonunuliwa kwa franka nyingi”.

Katika mgahawa wa vyakula pembeni, mrasibu analaani hasara aliyopata katika wiki mbili zilizopita.

” Tunanunua chakula ambacho kitatumiwa kwa siku moja. Ni muda wa asubuhi ambapo tunapata matatizo mengi sababu hatuwezi kuuzisha maziwa. Tulikuwa na uwezo wa kuuzisha hadi lita 15 kwa siku lakini tunalangua tu lita tano ili kujiepusha na hasara ” alihakikisha.

Katika familia ambazo zina mazoea ya kununua vitu vinavyohidhiwa ndani ya frije au jakofu, bidhaa hizo zinaoza siku moja badaye.

Kwa mjibu wa ushuhuda uliotolewa na wandishi wetu, umeme unakatika kwa angalau mara nne kwa siku kabla ya kukatika kwa muda mrefu wakati wa usiku.

” Hatuelewi umuhimu wa Regideso “, wanalaani.

Regideso bado haijajieleza kuhusiana na madai hayo ya wakaazi.

Previous Burundi : bei ya mbolea ya kizungu yapandishwa
Next Cibitoke: wanajeshi sita wasimamishwa baada ya kupurukushana na Imbonerakure