Cibitoke: wanajeshi sita wasimamishwa baada ya kupurukushana na Imbonerakure

Cibitoke: wanajeshi sita wasimamishwa baada ya kupurukushana na Imbonerakure

Wanajeshi hao sita walikuwa wakifanyia kazi kwenye kituo cha Ruhagarika . Ni katika tarafa ya Buganda ndani ya mkoa wa Cibitoke kaskazini magharibi mwa Burundi karibu na mto wa Rusizi unaotenganisha Burundi na jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Watano kati ya hao wanazuiliwa katika gereza la kamshena ya polisi ya mkoa huo tangu tarehe 13 septemba baada ya kupurukushana na wajumbe wa tawi la vijana wa wafuasi wa chama tawala cha CNDD FDD. Mwendeshamashataka mkoani Cibitoke anasema kuwa uchunguzi unaendelea. HABARI SOS Medias Burundi

Wanajeshi hao ni wanafanyia kazi katika bataliani ya 112 ya Cibitoke. Walikamatwa baada ya tukio la tarehe 13 septemba katika eneo hilo.

” imbonerakure walikuwa na lengo la kupeleka ng’ombe zaidi ya kumi nchini DRC ( jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) wakipita katika mto Rusizi. Wanajeshi waliokuwa kwenye ulinzi katika mto huo waliwakata kabla ya kupiga risasi. Imbonerakure mmoja alijeruhiwa vikali.

Vyanzo katika jeshi vilisema kuwa ” walijihami”.

” ni kundi la wezi linaloundwa na Imbonerakure ambalo linawasaidia wafanyabiashara kuingiza au kutoa biashara ya magendo ambao walianza kuwapiga risasi wanajeshi hao wanaofanya ulinzi kwenye mto wa ” Rusizi ” wanahakikisha.

Mshangao na maelezo ya mahakama

Vyanzo vingi vya ndani vinasema kuwa ” walishangaa “.

” Vipi wanaweza kusimamisha wanajeshi wakati walipokuwa wakifanya kazi yao ?Vyanzo vyetu vinajiuliza.

Mwendeshamashataka anasema kuwa uchunguzi unaendelea bila hata hivyo kutoa maelezo mengi.

Mkimbizi atoroka

Mmoja kati ya wafungwa sita alitoroka usiku wa tarehe 16 kuamkia 17 septemba, mashahidi walithibitisha. Jela la kamishna ya polisi ya mkoa wa Cibitoke linawapa hifadhi angalau wafungwa 170 ambao wanaishi katika mazingira mabaya huku hali hiyo ikiathiriwa zaidi na msongamano na ukosefu wa vyakula ambao ulisababisha vifo vya wafungwa wawili mwezi septemba kulingana na vyanzo vyetu.

Eneo ambako risasi hizo zilisikika, linatumiwa kama njia ya kusafirisha biashara ya magendo kati ya Burundi na Kongo tangu miaka mingi kwa mjibu wa vyanzo.

Previous Bujumbura : kazi zavurugika kutokana na umeme unaokatika mara kwa mara
Next Burundi : ni lazima iwepo sera ya misharaha inayovutia ili kuwazuia waganga kwenda nje ya nchi (Chama cha wafanyakazi)