DRC : siku chache baada ya muhula wake kumalizika, kikosi cha EAC chaomba kuongezewa muda
Kikosi cha kanda ya jumuiya ya Afrika mashariki EAC kilichotumwa katika mkoa wa kivu kaskazini (mashariki mwa DRC) kutokana na waasi wa M23 kudhibiti maeneo kadhaa, kinaomba kupewa muda wa ziada, hadi tarehe 8 septemba ijayo. HABARI SOS Médias Burundi
Ombi hilo lilitolewa na Aden Duale, katibu katika wizara ya ulinzi nchini Kenya.
” Tuliomba serikali ya DRC kujipanga kwa ajili ya kuongeza muhula wa kikosi cha kanda ya EAC hadi baada ya tarehe 8 septemba ili kudumisha matunda ya kikosi hicho cha kikanda “, alifahamisha mwishoni mwa wiki iliyopita.
Nchi wanachama wa EAC ziliamuru jumatano tarehe 31 mai wakati wa mkutano wa kilele wa 21 wa ma rais wa nchi za EAC kuongeza muhula wa kikosi cha EAC nchini DRC hadi 8 septemba 2023. Muhula huo ungemalizika alhamisi tarehe mosi juni.
Marais wawili, William Ruto wa Kenya na Evariste Ndayishimiye wa Burundi ambaye pia ni mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika mashariki walihudhuria mkutano huo uliofanyika mjini Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi.
Kwa kipindi cha siku tatu, washiriki walifanya tathmini ya uwendeshaji wa operesheni za kikosi cha kanda ya EAC katika mkoa wa Kivu kaskazini.
” Mkutano huo uliamuru wakusanywe pamoja waasi wa kundi la M23 eneo la Rumangabo (Kivu kaskazini) chini ya uangalizi wa mjumbe wa kikosi cha kikanda na FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo). Mbali na hayo, uamzi wa kuondoka kwa kikosi cha EAC unaweza kuchukuliwa katika kikao cha makadirio ki nachopangwa kufanyika juni 15 ” yalisomeka katika tamko la kuhitimisha mkutano wa Bujumbura.
Wananchi wakaazi wa mkoa wa Kivu kaskazini na mashirika ya kiraia, wanaendelea kutofautiana kuhusu matokeo ya harakati za kikosi cha kanda ya EAC nchini DRC, mbali na kikosi cha wanajeshi wa Burundi kilichowekwa katika wilaya ya Masisi.