Rugombo : watu wawili, mke na mumeo wapatikana wakiwa maiti nyumbani kwao

Rugombo : watu wawili, mke na mumeo wapatikana wakiwa maiti nyumbani kwao

Tharcisse Nsanzamahoro (miaka 49) na mke wake Thérèse Nzohabonimama, miaka 52 walipatikana wakiwa maiti nyumbani kwao jumapili hii asubuhi kwenye transversale 3 tarafani Rugombo katika mkoa wa Cibitoke (kaskazini magharibi mwa Burundi). Familia ya wahanga hao inaomba waliohusika na mauwaji hayo watafutwe na wakamatwe. Mkuu wa tarafa anathibitisha habari hizo na kuzidi kuwa uchunguzi tayari umeanzishwa. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mujibu wa ushahidi iliyotolewa na jirani, wawili hao ambao walikuwa na watoto nane, walichangia vinywaji na marafiki siku moja kabla katika mgahawa.

Wapendanao hao waliotuhumiwa uchawi kwa kipindi kirefu, huenda walitumia kinywaji chenye sumu .

” Huenda kuna mtu aliyetaka kulipiza kisasi, sababu watu hao waliofariki walisotwa kidole mara nyingi na kuhusishwa katika visa vya uchawi ambavyo vilisababishwa vifo vingi”, alisisitiza jirani huyo.

Kulingana na chanzo cha usalama, uchunguzi unaoendelea umepelekea watu watatu kukamatwa. Kwa sasa wanahojiwa na kuzuiliwa katika gereza la tarafa ya Rugombo.

Watu wa karibu na wahanga wanalaani ” mauwaji hayo ya watu wawili wasiokuwa na hatia ” na kuomba vipimo vifanyike ili kutambua kilichosababisha vifo vya watu hao.

Mkuu wa tarafa ya Rugombo anathibitisha taarifa hizo na kuzidi kuwa uchunguzi wa kina unaendelea ili kukamata waliohusika.

Gilbert Manirakiza anaomba wananchi kushirikiana na polisi na vyombo vya sheria wakati huu wa uchunguzi na kujizuia na mwenendo wa kujichukulia sheria mikononi.

Previous Musigati : amri ya kung'oa heka 50 za mashamba ya miwa
Next DRC : siku chache baada ya muhula wake kumalizika, kikosi cha EAC chaomba kuongezewa muda