Musigati : amri ya kung’oa heka 50 za mashamba ya miwa
Mkuu wa tarafa alichukuwa uamzi wa kupiga marufuku miwa katika bonde la tarafa ya Musigati mkoa wa Bubanza (magharibi mwa Burundi). Zao hilo litatoa nafasi kwa mazao mengine ya vyakula, kwa mujibu wa viongozi wa mkoa. Wamiliki wa mashamba ya miwa wanasema kuwa wamevunjika moyo. HABARI SOS Médias Burundi
Mkuu wa tarafa anaeleza kuwa anataka kukabiliana na njaa ambayo inakabili familia mkoani Bubanza.
” Ni kuondoa mashamba yote ya miwa ndani ya bonde la Musigati na kupanda eneo hilo mahindi, maharagwe, na mimea mingine ya mabondeni “, alibaini gavana wa mkoa wa Bubanza katika mkutano tarafani Musigati.
Hakika ni heka 50 za mashamba ya miwa zinazohusishwa. Na hatua hiyo ilianza kutekelezwa tangu ilipotangazwa, kwa mujibu wa wakaazi.
” Uongozi wa tarafa uliwaalika Imbonerakure ( wajumbe wa tawi la vijana wafuasi wa chama cha CNDD-FDD) kutekeleza uamzi huo. Walilata , kung’oa na kuharibu mashamba ya miwa katika mto wa Nyamugerera , waliripoti mashahidi.
Na katibu wa chama cha CNDD-FDD alishindilia.
” Hawaelewi kuwa muwa unaleta mavuno mara moja kwa mwaka. Mazao mengine yanaleta mavuno angalau mara mbili. Kwanza pesa inayotokana na zao hilo huchangia katika kitendo cha kuparika. Uamzi huu hawutabadilika ” alibaini Alexandre Ngoragoze.
Fundi wa kilimo tarafani Musigati anasema zao hilo lililopewa jina moja na tarafa hiyo katika lugha ya taifa ( Umusigati =muwa ) litapelekwa katika maeneo mengine na ambako kuna maji.
Wakaazi wanadai kuwa ni hatua ambayo hawakufikiria. Wanasema zao la miwa lilikuwa na faida : Shamba la miwa la ukubwa wa mita mraba 20 , linaweza kuingiza kitita cha 350.000 zikiwa ndogo. Kitita hicho kinatocha ili kuanzisha biashara ndogo yenye faida kwa familia na katika uchumi wa tarafa “, wanadai wakulima.