Burundi : Imbonerakure zapewa sifa na kuhitajiwa

Burundi : Imbonerakure zapewa sifa na kuhitajiwa

Rais wa Burundi ametoa sifa na kupongeza Imbonerakure (wajumbe wa tawi la vijana wafuasi wa chama cha CNDD-FDD, chama tawala) kwa jukumu lao katika kulinda mipaka ya nchi yake. Evariste Ndayishimiye pia aliwatolea mwito kuongeza kasi katika doria za usiku akidai kuwa ” pale ambako kuna Mungu, na shetani pia anakuwepo “. Ilikuwa katika awamu ya saba ya sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya siku maluum ya Imbonerakure. HABARI SOS Médias Burundi

Sherehe hizo zimefanyika kwenye makao makuu ya mkoa wa Makamba kusini mwa Burundi. Rais wa Burundi amekuwa akisubiriwa sana pamoja pia na hutba yake. Alisifu jukumu la vijana wafuasi wa chama tawala cha CNDD-FDD katika kulinda mipaka ya nchi.

” Burundi inalindwa sababu tuko na Imbonerakure. Ambaye hakubali, athubutu kuingilia mipaka yetu. Ataelewa ” , amefahamisha Bwana Neva mbele ya Imbonerakure, watoto kutoka familia za wafuasi wa chama tawala, viongozi, wawakilishi wa chama pamoja na wajumbe kutoka nchi za Afrika.

Kuhitajika

Akijieleza katika lugha ya taifa, Kirundi, rais Ndayishimiye amejipongeza kwa uwepo wa Imbonerakure wanaofanya doria za usiku na kuwatolea mwito kuzidisha kasi.

” Imbonerakure wako na uwezo wa kulinda kila sehemu ndogo ya mipaka yetu. Hakuna anayeweza kupita pembeni. Ninawaomba kusalia katika tahadhari sababu pale ambapo kuna Mungu, na shetani pia anakuwepo. Imbonerakure ambaye hafanyi doria usiku mzima hana sifa ya kupewa jina hilo. Imbonerakure ambaye ana woga hana sifa ya kupewa jina hilo”, amesisitiza rais wa Burundi.

Umoja wa mataifa na umoja wa ulaya

Kwa mujibu wa rais wa Burundi, umoja wa mataifa pamoja na umoja wa ulaya waliharifu sura ya wafuasi wa tawi la vijana wa chama tawala baada ya kuonyesha upinzani wao dhidi ya kuivamia Burundi na kufanyika mauwaji nchini Burundi.

” Umoja wa mataifa, umoja wa ulaya na baadhi ya nchi ambazo bado zinavumilia sera ya kutawaliwa ziliharibu sura ya Imbonerakure ( 2016) baada ya kukataa mauwaji yasifanyike dhidi ya warundi na kupinga uvamizi dhidi ya Burundi “, amehakikisha muasi hiyo wa zamani wa kihutu. Kama kumbusho, UN ilitaja Imbonerakure kama ‘ waasi” na kifaa cha ukatili kinachotumiwa na utawala wa CNDD-FDD.

Udanganyifu

Kulingana na rais Evariste Ndayishimiye, Imbonerakure maskini haingekuwepo katika nchi yenye utajiri wa asilia.

” Umoja ni nguvu. Tuko na bahati sababu niliweza kusimamisha wizi wa rasilimali yetu ya asili kuelekea nchi za nje kabla ya kuchelewa. Kwa sasa, tutaanza kutengeneza mali yetu ya asili sisi wenyewe. Tuna uwezo wa kijihudumia [….], aliwambia mbele ya umati wa watu asifa huyo anayeongoza nchi ya kwanza kabisa masikini duniani ambayo mamlaka ya nchi ya ugavi wa maji na umeme ikiwa haina uwezo wa kuhudumia wateja wake wa mji mkuu wa kiuchumi hususan.

Utawala wa milele ?

Rais Neva amepongeza uwepo wa watoto wadogo katika sherehe hizo. Ni watoto kutoka familia za wafuasi wa chama cha CNDD-FDD. Walipewa jina na ” Ibiswi vy’inkona ( Tai au nembo ya chama tawala)”.

” Ninafurahi kuona ” Ibiswi vy’inkona hapa. Ni dalili kuwa munawaandaa warithi wenu sababu 2060 ni wawo ambao wataridhi utawala. Nyinyi hata 2040 mtakuwa wazee, amebaini rais huyo ambaye hutba yake imependwa na wafuasi wa kikundi hicho za zamani za kihutu.

Rais Neva amepongeza Imbonerakure ambao waliboresha uwezo wao wa kufanya gwaride kama walivyotakiwa mwaka jana.

Sasa, ni mwaka wa saba mfululizo ambapo chama cha CNDD-FDD kinaadhimisha siku maluum ya Imbonerakure. Hakuna chama kingine cha kisiasa kinachoruhusiwa kufanya gwaride katika nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki, hata kile ambacho asili ni moja , kutoka kikundi cha waasi wa kihutu.

Nchi nyingi za Afrika ziliwatuma wajumbe wake katika sherehe za jumamosi hii au kutoa ujumbe wa kirafiki na ushirikiano.

Previous Burundi : Imbonerakure zapewa sifa na kuhitajiwa
Next Musigati : amri ya kung'oa heka 50 za mashamba ya miwa