Gitega : watu saba wapewa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja na miwili jela kwa kuhusika na ushoga
Kati ya wale saba walioadhibiwa kwa kuhusika na ushoga, watano walikatiwa kifungo cha miaka miwili jela. Wawili mwaka mmoja jela. Wengine 18 waliachiliwa na mahakama kuu ya Gitega (kati kati mwa Burundi). Upande wa utetezi wanafahamisha kuwa watakata rufaa. HABARI SOS Médias Burundi
Kesi hiyo ilikatwa tarehe 22 agosti iliyopita kwa mjibu wa mawakili. Waliodhibiwa wanatumika au ni wajumbe wa shirika la ” Muco”. Ni shirika hilo la ndani lililoandaa warsha wakati wahusika hao walipokamatwa na polisi pamoja na idara ya ujasusi katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega mwishoni mwa mwezi februari iliyopita 2023.
” Watuhumiwa 18 walipatikana bila hatia, watano walipewa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela wakati wawili wengine watatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela”, alieleza mmoja kati ya mawakili wao.
Watu saba wanaojumuika katika shirika la ” Muco” walipatikana na kosa la ushoga na kushawishi watu kutumia vileo ” vyanzo katika idara ya sheria vilihakikishia SOS Médias Burundi.
Kifo cha mmoja aliyepatikana bila kosa
Mevin Shurweryimana alifariki usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa iliyopita. Alikuwa akipata matibabu kwa siku kadhaa kwenye hospitali ya kikanda ya Gitega. Vyanzo vya karibu na faili vinatuhumu idara ya magereza pamoja na korti ya mkoa kukataa kumpa idhini ya kwenda hospitali kwa wakati.
” Mkuu wa gereza pamoja na korti ya mkoa walikataa kumpa ruhsa ili aweze kujitibisha kwa wakati inaofaa wakati akiumwa homa ya ini aina ya B. Wakati walipompa ruhsa, walikuwa wamechelewa, afya yake ilikuwa imedhofika “, vyanzo viliambia SOS Médias Burundi.
Mhamasishaji huyo wa shirika la ” Muco “, mwenye asili ya eneo la Mugutu ( Gitega) atazikwa jumanne hii kwa mjibu wa vyanzo katika familia yake.
Kiongozi mkuu anayehusika na maswala ya magereza, msemaji wa mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri na kiongozi wa gereza la Gitega hawakupatikana ili wajieleze juu ya madai hayo. Hawakujibu ujumbe ambao tuliwaandikia kupitia WhatsApp.
Watu wengine waliripoti mahakani wakiwa huru. Hadi jumatatu jioni, wafungwa 14 ambao wangetakiwa kuachiliwa huru kwa amri ya mahakama kuu ya Gitega, walisalia katika gereza la mji mkuu wa kisiasa. Mmoja kati ya mawakili alilaani ukiukwaji wa sheria”.
Mashoga, watu waliolaaniwa kwa mujibu wa rais Neva
“[…] mashoga wa Burundi hata wale wanaoishi nje ya nchi, popote pale walipo, na hata marekani, wanatakiwa kupingwa na watu waliolaaniwa”, alisisitiza Evariste Ndayishimiye wakati wa kikao na wabunge mwanzoni mwa mwezi machi, bila kutaja kundi lililokamatwa katika mji wa Gitega, siku chache kabla.
Tarehe 15 agosti iliyopita, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka wa 125 ya kanisa katoliki nchini Burundi, alikuwa wazi katika maneno yake mbele ya muwakilishi wa baba mtakatifu.
” Licha ya watu wa nchi za magharibi kuingiza ukiristu nchini Burundi, tunalaumu kuona wanapigia debe ushoga, kuporomosha mimba na kutengeneza silaha za nuklia na kuwamalizia maisha watu mahtuti”, alisisitiza.
Upande wa utetezi ulisema kuwa utakata rufaa.
Hadi disemba 2022, nchi 68 duniani zilifanya ushoga kuwa kosa la jinai . Nchi hizo zinapatikana barani Eshia , Afrika na mashariki ya kati. Angalau nchi 11 kati ya hizo, zinatoa hukumu ya kifo dhidi ya mashoga. Nchini Burundi, wanapewa adhabu ya kifungo cha hadi miaka miwili jela na faini.