RDC-Burundi : rais Neva anaendelea kutafuta mikataba kwa ajili ya FDNB*
Burundi na jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo zilisaini makubaliano katika sekta ya ulinzi tarehe 28 agosti mjini Kinshasa mji mkuu wa RDC (jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo). Marais hao wawili wa Burundi na Kongo waliosaini makubaliano hayo walidai kuwa yatasaidia kurejesha amani mashariki mwa Kongo. Tathmini za watu huru zinaonyesha mashaka. HABARI SOS Médias Burundi
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye aliwasili jumapili iliyopita mjini Kinshasa mji mkuu wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya ziara rasmi ya siku mbili.
Baada ya kupokelewa na waziri mkuu wa Jean-Michel Sama Lokonde kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa N’djili, rais Ndayishimiye alichangia chakula cha jioni na rais Félix Tshisekedi kwenye ikulu ya Mont Ngaliema.
Shughuli rasmi ya kazi ilifanyika jumatatu kwenye kasri la Palais de la nation.
Baada ya mkutano wao wa ana kwa ana, ma rais hao wawili waliongoza kikao na wandishi wa habari wakiwa pamoja kuhusu mkutano wao huo ambao ulifanyika wiki chache baada ya kikao cha mwisho cha viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) kilichofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi.
Harakati za FNDB
” Kikosi cha Burundi kinachohudumu Kivu kaskazini hakijatoa nafasi kwa adui wa wananchi na hali hiyo inaonyesha uhusiano mzuri kati ya nchi zetu na ujirani mzuri kati ya wananchi wetu. Ninatoa wito kwa vikosi vingine vya kanda hii vilivyotumwa nchini DRC kufanya kama wanajeshi wa Burundi “, rais Neva alisifu jeshi la nchi yake.
Tahadhari ya Tshisekedi
Akitoa majibu, Félix Tshisekedi, alitahadharisha baadhi ya vikosi vya kigeni vinavyounga mkono waasi wa M23 kwa kuwaruhusu kukusanya ushuru, kwa mjibu wake.
” Tunawaangalia kwa karibu wanajeshi wa EAC lakini kuna kasoro kwa baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha kikanda wanaosaidia waasi. Tuna matumaini kuwa kanda itashughulikia swala hilo na kutafuta njia ya suluhu inayodumu”, alisisitiza rais wa Kongo .
Ushirikiano wa kijeshi
Baada ya kuzungumza na wandishi wa habari mbele ya ikulu ya Palais de la Nation, ma rais hao wawili walisaini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi.
Kuridhika kwa Tshisekedi
Rais wa Kongo alisema kuridhika na makubaliano hayo ambayo yatawezesha pia nchi hiyo kubwa jirani magharibi ya Burundi kuendelea kiuchumi kulingana na rais huyo.
” Burundi ni rafiki yetu wa tangu jadi. Wananchi wetu wanachangia vitu vingi kupitia mipaka ya pamoja inayotuunganisha. Kupata ushirikiano wa kijeshi na Burundi ni faida “, alihakikisha bwana Tshisekedi.
Maoni tofauti
Wangalizi pamoja na wakaazi wanaendelea kukosoa uwajibikaji mbaya wa vikosi vya kigeni nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
” Ushirikiano huo hautakuwa na matokeo yenye manfaa kwa raia wa Kongo sababu rais wa Burundi ni mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika mashariki iliyotuma kikosi mashariki mwa Kongo. Ni kikosi ambacho hakikufanikisha jukumu lake ” alisema Emmanuel Binyenye , mtathimini wa siasa za Kongo.
Kulingana na baadhi ya wakaazi waliowasiliana na SOS Médias Burundi, FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) linatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha badala ya kusubiri msaada kutoka kwa kanda hii.
” Matatizo ya nchi yetu ni matatizo yetu, na ni jukumu letu kuyashughulikia. Hakuna kikosi cha kigeni ambacho kitamumaliza adui bila mchango wetu ” , alidai mwananchi mkaazi wa eneo la migogoro ya silaha kwa miaka mingi ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini.
Mkaazi mwingine wa makao makuu ya mkoa anasema hiyo ni danganya toto.
” Kushirikiana na nchi jirani kwa mjibu wetu ni kutuzubaza. DRC inatakiwa kutafuta namna ya kudhibiti madui wa amani na sio kutafuta misaada kwa vikosi vya nje” alilaumu mkaazi wa mjini Goma mwenye umri zaidi ya miaka 40.
Utata
Hadi sasa, makubaliano hayo hayako wazi. Rais wa Burundi alisema tu kuwa kikosi maluum kinaweza kupelekwa kwa ajili ya kusaidia Kongo kurejesha amani na usalama katika eneo lake la mashariki.
Akiongoza EAC tangu julai 2022, rais Ndayishimiye anahusishwa katika mchakato wa amani wa Nairobi ( Kenya ) kwa ajili ya kurejesha amani na utulivu katika mkoa wa mashirika mwa DRC .
Jeshi la Burundi lilitumwa kupitia kikosi cha kanda ya EAC likiwa na wanajeshi 1000 kwa ajili ya kupigana na waasi wa M23 katika mkoa wa Kivu kaskazini na waasi wa wa ndani pamoja na makundi ya silaha yenye asili ya Burundi ndani ya Kivu kusini.
Jeshi la FNDB linahudumu kwenye ardhi ya Kongo chini ya mikataba miwili : mkataba wa ushirikiano kuhusu sehemu ya wanajeshi waliotumwa eneo la Kivu kusini pamoja na mkataba wa kikanda kwa kikosi kinachopatikana eneo la Kivu kaskazini.
FDNB *: Jeshi la Burundi
About author
You might also like
Kesi-Bunyoni : sheria nchini Burundi yafunga akaunti za waziri mkuu wa zamani
Benki kuu ya Burundi BRB ( benki ya jamuhuri ya Burundi) ilitoa amri kwa mashirika ya fedha yote ili yasiruhusu kuondoa au kuweka pesa kwenye akaunti za waziri mkuu wa
Burundi : nchi imepata mwendeshamashtaka mkuu mpya
Ni Léonard Manirakiza, ameidhinishwa jumanne hii na baraza la seneti. Wanaharakati wanasema kuwa hawataraji mambo makubwa kutoka kwake lakini wameamuru kujizuia kueleza chochote. HABARI SOS Médias Burundi Léonard Manirakiza ameidhinishwa
Bujumbura: kukamatwa na kufuatiwa na kuwekwa kizuizini kwa maafisa wa kampuni ya kibiashara na utengenezaji
Meneja mkuu wa kampuni ya biashara na utengenezaji bidhaa iliyoko Bujumbura, jiji la kibiashara la Burundi, na msaidizi wake wamekuwa wapangaji wa gereza kuu la Bujumbura linalojulikana kwa jina la