Dzaleka (Malawi) : wakimbizi watatu wafariki dunia baada ya kufanyiwa mateso

Dzaleka (Malawi) : wakimbizi watatu wafariki dunia baada ya kufanyiwa mateso

Watu hao ni raia wawili wa Burundi na mwingine mwenye asili ya Rwanda. Walikuwa walikamatwa katika msako wa wakimbizi wanaoishi mijini na kuzuiliwa ndani ya gereza kuu ya Maula. Viongozi wa wakimbizi katika kambi ya Dzaleka, wanaomba uchunguzi huru ufanyike. HABARI SOS Medias Burundi

Jumapili iliyopita katika usiku majira ya saa nne za usiku, gari iliwasili ndani ya kambi ya Dzaleka nchini Malawi. Kulingana na wakimbizi ilikuwa ikiwaleta wakimbizi hao wakiwa katika hali mbaya.

” Tulikuwa tunalala tukasikia fujo. Tulitoka nje kuangalia kinachofanyika. Tuliona watu wengi wanaozunguka gari ya polisi aina ya pick-up. Wakati tuliposogea, tuliona wakimbizi nane, warundi watano pamoja na wakimbizi watatu kutoka Rwanda, waliokuwa wamelala pembeni ya gari hiyo”, mashahidi wanaeleza.

Na kulaani kuwa : ” wakimbizi hao walikuwa hawana uwezo wa kusema isipokuwa tu kupiga kilele kutokana na maumivu, walikuwa hawawezi hata kujitingisha. Walionekana kama watu waliochoka sana na kufanyiwa mateso.

Polisi na HCR hawajakubaliana

Polisi ilieleza ofisi ya HCR ya kambi ya Dzaleka kuwa watu hao waliachiliwa huru kutoka gereza kuu ya Maula na kwamba wanatakiwa kupokelewa na kurejeshwa ndani ya kambi hiyo.

Ofisi ya HCR ilikataa kuwapokea ” watu hao waliokuwa katika hali mbaya”.

” Tunamushukuru mwakilishi wa HCR ambaye amekuwa na utu na hivyo kukataa kupokea watu hao. Aliambia polisi kuwa hawezi kupokea watu mahtuti, hivyo polisi inatakiwa kwanza kuwatibisha na kuwaleta wakati wa mchana hapana usiku”, viongozi wa kijamii waliokuwepo wakati wa tukio walitoa ushahidi huo.

Baada ya mazungumzo marefu, polisi iliamuru kurudi nyuma na wakimbizi hao na ” kuwapeleka kwenye hospitali”

Vifo vya wanaume watatu

” Watu hao walipokelewa kwenye hospitali eneo la Dowa si mbali na kambi. Asubuhi yake, tulishituka kwa kupata taarifa mbaya kuwa watu kati ya hao walifariki dunia. Watano wengine walipelekwa kwenye hospitali ya kanda ya Dowa kwa ajili ya matibabu ya dharura”, wakimbizi walieleza.

Tuhuma kali

Mmoja kati ya wakimbizi hao ambaye bado yuko hai, aliweza kutoa maneno makali akilazwa katika hospitali.

” Tulifanyiwa mateso. Walitunyima chakula kwa kipindi kirefu ndani ya gereza la Maula. Walitudunga sindano. Walitutuhumu kupinga amri ya kuondoka nje ya vituo vya miji”, alikumbuka akiwa mdhaifu.

Viongozi wawili wa kambi ya Dzaleka, raia wa Burundi na Rwanda waliwasili kwenye hospitali ili kuomba maiti zao lakini uongozi wa kituo hicho cha afya ulikataa kuwakabidhi miili hiyo.

Hasira kamili

” Tunaomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kugundua chanzo cha vifo hivyo. Waliohusika na mateso hayo wanatakiwa kuadhibiwa kwa mjibu wa sheria. Tunasikitika, haki zetu haziheshimiwi. Kama kuna makosa yaliyofanywa na mkimbizi, ni lazima afikishwe mbele ya vyombo vya sheria”, walisema.

Mwezi aprili iliyopita, serikali ya Malawi ilitoa ilani ya mwisho kwa wakimbizi wanaoishi katika vituo vya mijini kurejea ndani ya kambi iliojaa ya Dzaleka kwenye umbali wa kilometa takriban 40 ya mji mkuu Lilongwe.

Mwishoni mwa mwezi mei, waziri anayehusika na usalama wa ndani alifahamisha kupitia radio-televisheni ya taifa hilo kuwa zaidi ya wakimbizi 400 na waomba hifadhi wakiwemo watoto walikamatwa katika operesheni ya polisi iliyofanyika katika kata za mji mkuu Lilongwe kwa ajili ya kuwakamata wakimbizi ambao hawakuitikia wito.

Wajumbe wa jamii za warundi, wakongomani na raia wa Rwanda wanaoishi katika kambi ya Dzaleka wanasema kuwa huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kuomba viongozi wa nchi ya Malawi na HCR kusimamisha vitendo hivyo.

Kambi ya Dzaleka inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi elfu 50 kutoka mataifa mengi ya bara la Afrika wakiwemo raia elfu 11 wenye asili ya Burundi.

Previous RDC-Burundi : rais Neva anaendelea kutafuta mikataba kwa ajili ya FDNB*
Next Burundi : hutba ya rais Neva itaimarisha vitendo vya uhalifu vinavyotekelezwa na Imbonerakure, kwa mujibu wa Carina Terksakian