Burundi : hutba ya rais Neva itaimarisha vitendo vya uhalifu vinavyotekelezwa na Imbonerakure, kwa mujibu wa Carina Terksakian
Rais Evariste Ndayishimiye jumamosi tarehe 26 agosti 2023, alisifisu jukumu la Imbonerakure katika kufanya doria za usiku na kulinda mipaka. Kwa mujibu wa Carina Terksakian, mtafiti mshirika katika shirika la IDHB linalotetea haki za binadamu nchini Burundi, hutba hiyo itatoa msukumo kwa wajumbe wa tawi la vijana wafuasi wa chama tawala kufanya vitendo vya uhalifu na kukiwa na hatari watu kukamatwa kinyume cha sheria, visa vya kunyanyasa watu kutokea na hata mauwaji kuongezeka. HABARI SOS Médias Burundi
Rais wa jamuhuri alitoa hutba ya kukanganya kuhusu Imbonerakure. Tangu alipoingia madarakani, mara nyingi aliwasihi Imbonerakure kujihusisha zaidi na shughuli za maendeleo na kuachana kabisa na harakati za ” usalama” pamoja na visa vya uhalifu dhidi ya mahasimu wao. Ni matamshi yanayoridhisha kwa jumla. Lakini jumamosi iliyopita akiwa katika shughuli za siku maluum za Imbonerakure, ni kama alirudi nyuma kwa kuwasukuma Imbonerakure kulinda usalama wa mipakani na kufanya doria za usiku. Ni matamshi yanayosababisha wasi wasi sababu watu wote wanafahamu matokeo ya kazi za Imbonerakure kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, alisema SOS Médias Burundi Carina Tertsakian katika mahojiano maluum na SOS Médias Burundi.
” Aina hiyo ya ujumbe kutoka kwa rais wa nchi utawafanya (Imbonerakure) kuongeza visa vya uhalifu na unaweza kusababisha hata visa vya watu kukamatwa kinyume cha sheria kuongezeka, visa vya watu kukamatwa vibaya na hata mauwaji ” anahofia hayo afisa huyo anayehusisha na maswala ya haki za binadamu kwa zaidi ya miaka 25 katika eneo la maziwa makuu ya Afrika .
Kujichukulia sheria mikononi
Bwana Ndayishimiye alitahadharisha pia washirika wake ” wanaokula rushwa”. Alihakikisha kuwa ” nitawakabidhi wananchi ili wawape adhabu wenyewe, sintasubiri watu waingie mitaani kuandamana “, akisisitiza kuwa, uasi wa wananchi dhidi ya viongozi ni matokeo ya shughuli za viongozi ambao hawaheshimu haki za wananchi”.
” Burundi iko na idara ya sheria hata kama inakabiliwa na changamoto nyingi. Iwapo mwananchi au mtu yoyote anapofanya kitendo chochote cha rushwa au kosa lolote, ni jukumu la sheria kufanya kazi yake. Viongozi wa kisheria wanatakiwa kufanya uchunguzi na iwapo ushahidi unatosha, muhusika anatakiwa kuwekwa mbele ya vyombo vya sheria. Kumukabidhi mtu kwa wananchi, sio suluhu. Badala yake, ni kutoa kipau mbele kwa watu kujichukulia sheria mikononi. Rais angetakiwa kuwajibika katika kuimarisha mfumo mzima wa sheria na kurejesha uhuru wake na kuboresha mfumo huo”, alidai Carina Tertsakian.
Haki za binadamu
Katika hutba yake, rais aliongelea kulinda haki za binadamu. Ni jambo zuri, aliendelea kusema mtafiti huyo katika shirika la IDHB.
” Lakini alifanya nini katika kulinda haki za binadamu ? Hutba nzito au kuwafuta kazi viongozi wa ndani haitoshi. Iwapo anataka wananchi wa Burundi waweze kuamini ahadi zake, angetakiwa kumaliza hali ya kutoadhibu viongozi wa juu waliofanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu tangu miaka kadhaa. Hata washirika wa kimataifa wa Burundi wataanza kuamini iwapo baadhi ya viongozi wakuu watawajibishwa mbele ya sheria “, alimalizia.
Hutba hiyo iliyochukuliwa na wangalizi wa ndani na nje kama mapungufu katika ahadi yake ya kukabiliana na ukiukwaji wa haki za binadamu na kutovumiliana kisiasa, ilisifiwa na kupokelewa vizuri na wafuasi wa kikundi hicho cha zamani cha waasi wa kihutu cha CNDD-FDD, kilichogeuka chama cha tawala mwaka wa 2005 kutokana na makubaliano ya amani na maridhiano ya Arusha agosti 2000..