Cibitoke-Gitega : wazazi wazidiwa na kupanda kwa bei ya vifaa vya shule
Siku chache kabla ya mwaka wa masomo 2023-2024 kuanza, wazazi pamoja na wanafunzi mkoani Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi) na Gitega (mji mkuu wa kisiasa kati kati mwa Burundi) wanashituka kutokana na kupanda kwa gharama ya vifaa vya shule. Bei ya vifaa vya shule ilipanda kwa zaidi ya asilimia 30 kwa kila kitu. Wazazi wanasema kuwa uwezo wao umezidiwa. Wanahofia kutokea idadi kubwa ya wanafunzi watakaoacha shule mwaka huu. HABARI SOS Médias Burundi
Baada ya kupata taarifa hizo, wandishi wetu walielekea katika baadhi ya soko mkoani Cibitoke ili kushuhudia hali ya mambo.
Daktari ya ukurasa mia moja inauzishwa franka 2500 wakati mwaka jana, bei yake ilikuwa franka 2000. Hali hiyo ya bei kupanda, ilishuhudiwa pia katika aina nyingine za daftari kala walivyogundua wandishi wetu eneo la Rugombo na kwenye makao makuu ya mkoa.
Sare za wanafunzi pia hazikuepukika na hali hiyo. Kwa sasa bei ni franka elfu 30 wakati mwaka jana bei ya sare za shule ilikuwa elfu 20.
Hali ni kama hiyo katika tarafa zote za mkoa wa Cibitoke kwa mujibu wa wandishi wetu.
Wazazi waliozungumza na SOS Médias Burundi wanasema kuwa ” hawana ulinzi ” dhidi ya mripuko huo wa bei ya vifaa vya shule.
” Vipi tutaweza kumudu hali hiyo. Mafuta ya gari, bidhaa za vyakula, na vinywaji vya BRARUDI, ….harafu pia vifaa vya shule !”alilaani mzazi mmoja aliyekuwa akitafuta vifaa kwa ajili ya watoto wake.
wazazi wanahofia kutokea idadi kubwa ya wanafunzi ambao wataacha shule mwaka ujao ukilinganisha na mwaka jana.
Gavana wa mkoa anahakikisha kuwa anafahamu hali hiyo na kutishia kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaopandisha bei. Carême Bizoza anatoa wito kwa wananchi kuwafichua watu wanaokwenda kinyume na bei rasmi.
Hali kadhalika mkoani Gitega : wazazi wapoteza matumaini
Hali hiyo ya bei kupanda inaripotiwa katika maeneo mengine ya nchi , kama mkoani Gitega, mji mkuu wa kisiasa.
Eneo hilo kama ilivyo mkoani Cibitoke, bei iliopanda hususan ni ya daftari, sare za wanafunzi na bidhaa zingine muhimu kwa ajili ya wanafunzi na kwa kiwango kikubwa.
Daftari ya ukurasa mia moja inanunuliwa 2500 wakati mwaka jana bei yake ilikuwa elfu mbili. Ile ya ukurasa 60 bei yake ilipanda kati ya franka 50 na 200 sarafu ya Burundi, walishuhudia wandishi wetu waliozunguka katika maeneo ya soko ya makao makuu ya Gitega.
Bidhaa zingine zikiwemo sare za wanafunzi na boxi za vifaa vya kukata mistari zilipanda bei pia. Bei ya boxi ya vifaa hivyo sasa ni 3000 badala ya 2000 sarafu za Burundi.
” Bei ni kubwa! sare ya mwanafunzi anayesoma kidato cha pili inauzishwa 18000 sarafu za Burundi. Hata mkoba wa kubeba mgongoni bei yake ilipanda hadi elfu 20000. Hautoni ni mkakati gani ambao tutatumia ili kugharamia masomo ya watoto wetu”, wazazi walipoteza matumaini.
Wafanyabiashara upande wao wanaeleza kuwa hali hiyo inasababishwa na thamani ya sarafu ya Burundi kushuka na uhaba wa sarafu za kigeni ili kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi.
Viongozi tawala wanaahidi kuwajibika na kuwaadhibu wanaopandisha bei.