Tanzania : viongozi wanahakikisha kuwa unyanyasaji dhidi ya wakimbizi wa Burundi unapuziwa
Wizara wa mambo ya ndani inahakikisha kuwa wakimbizi wa Burundi wananyanyaswa na polisi ndani ya kambi. Wizara hiyo inatoa ahadi ya kushughulikia swala hilo lakini haonyeshi ishara yoyote. Badala yake vitendo vya kuwadhalilisha wakimbizi vinaendelea kuongezeka. HABARI SOS Médias Burundi
Ni hali isiyoingia akilini. Katibu wa kudumu wa wizara ya mambo ya ndani nchini Tanzania inayohusika na maswala ya wakimbizi anahakikisha kuwa vitendo ” vya kuwadhalilisha wakimbizi wa Burundi ” vinatelelezwa na taasisi za serikali.
” Hakujakataa hilo. Polisi ilionekana katika vitendo vya aina hiyo, mara kadhaa haki za wakimbizi zikivunjwa. Baadhi wanapelekwa jela na badaye kuachiliwa huru, biashara zao zinapigwa marufuku, na misaada yao kusimamishwa “, alithibitisha Sudi Mwakibasi.
Ilikuwa katika mkutano wa kupeana maoni kuhusu hali ya wakimbizi pamoja na mashirika mengi ya misaada na wadau wengine wa sekta hiyo uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii ndani ya majengo ya ofisi ya OIM ( shirika la kimataifa kwa ajili ya wahamiaji) katika eneo la Makele kwenye umbali wa kilometa 5 kutoka kambi ya Nyarugusu kaskazini-magharibi mwa Tanzania.
” Watu wote wanafahamu hali hiyo, na baadhi tayari walilalamika kuhusu mateso wanayofanyiwa ndani ya magereza “, alizidi kusema huku akiahidi kushughulikia hali hiyo na kuibadilisha bila hata hivyo kuleta matumiani.
” Mara nyingi maelezo kuhusu sababu ya visa hivyo ni kutokana na kwamba wakimbizi walikataa kuitikia programu ya kuwarejesha makwao iliyoanzishwa kupitia makubaliano ya wajumbe wa kamati ya pande tatu. Lakini tutajaribu kuteleleza sheria na kusahihisha makosa hayo yaliyotokea “, alieleza.
Afweni kwa wakimbizi
Wawakilishi wa wakimbizi wenye uraia wa Burundi na Kongo waliohudhuria mkutano huo walipigwa na mshangao kwa kusikia kauli hiyo.
” Ni mafanikio makubwa kusikia kiongozi kama hiyo ambaye ana wajibu wa kulinda haki zetu akikiri na kukubali kuwa hazi zetu zinavunjwa, na kuomba radhi hadharani. Hakutajari mabadiliko yoyote lakini la muhimu ni kwamba nchi ya Tanzania inakubali jukumu lake katika ukiukwaji huo mkubwa”, walidai wakimbizi hao .
” Ni budi uchunguzi ufanyike na maafisa wanaohusika na vitendo hivyo waweze kuadhibiwa ili kuonyesha kuwa hawakuwa chini ya amri za viongozi wakuu wa Tanzania ” wawakilishi hao wa wakimbizi walisisitiza.
Migongano
Katika kambi za Nduta na Nyarugusu, wakimbizi walifikiria kuwa hali inakwenda kubadilika. Kwanza kabisa kuanzia jumatano hii baadhi walianza tena kufanya biashara zao ndogo dogo mbele ya makaazi yao. Majibu yaliwashangaza.
” Zaidi ya wakimbizi 20 walisimamishwa na polisi jioni ya jumatano wakati wakijaribu kuuzisha mandazi, mboga boga na matunda. Ni mgongano mkubwa baada ya ahadi ya muda mfupi ya mwakilishi wa wizara ya mambo ya ndani”, mashahidi wanalalamika.
Baadhi walikamatwa katika kijiji IV zone 12 na wanazuiliwa kwenye katika gereza la polisi maarufu kama ” station A”.
” Tulidhani kuwa huenda amri zilitolewa ili kutuhakikishia na kufungua biashara zetu ndogo na kuachia beskeli zetu za abiria ziweze kutembea ….tuliyoshuhudia kwa sasa, hayavumiliki ” walisema. Wakimbizi walitaja hutba ya bwana Mwakibasi kama ” maneno yaliyokuwa na tija “.
Mashirika mengi ya kiutu likiwemo shirika la Human Right Watch pamoja na kamati ya Afrika ya haki za binadamu yanalaani ukiukwaji huo wa haki za wakimbizi hususan wenye uraia wa Burundi mnamo miaka iliyopita nchini Tanzania. Mashirika hayo yanatoa idadi ya zaidi ya visa 170 vya wakimbizi kukamatwa kinyume cha sheria vikiwemo visa vya waliopotea mara moja .
Mashirika hayo ya kimataifa yalitoa wito kwa viongozi wa Tanzania kuacha vitendo hivyo na kuwapeleka mahakamani waliohusika.
Viongozi wa ndani katika kambi za Nduta na Nyarugusu wanahakikisha kuwa baadhi ya wakimbizi wanaamuru wenyewe kurudi nchini kwao kutokana na visa unyanyasaji na hivyo kuchagua ” kwenda kufa wakiwa nyumbani kwao” hali ambayo wanataja kama ni ” kuwarejesha nyumbani kwa nguvu “.
Tanzania inawapa hifadhi zaidi ya nusu ya wakimbizi wenye asili ya Burundi ambao wanasalia uhamishoni katika kanda hii, sawa na idadi ya 125000.